Saturday, November 28, 2020

MAYANGA AKUBALI YAISHE KWA ULIMWENGU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MARTIN MAZUGWA

KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga, amekubali yaishe baada ya kusema hataziba pengo la mshambuliaji, Thomas Ulimwengu, kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ulimwengu anayechezea klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden, ameshindwa kujiunga na wachezaji wenzake wa Stars kutokana na kutokuwa fiti kwa asilimia 100.

Akizungumza na BINGWA jana, Mayanga alisema alimtarajia nyota huyo kuja kuungana na wenzake, lakini imeshindikana kutokana na ripoti iliyotolewa na madaktari wa klabu yake kuwa ni majeruhi.

“Ni kweli Ulimwengu ni mchezaji muhimu katika timu kutokana na uzoefu aliokuwa nao, lakini nasikitika hatacheza michezo hii miwili kutokana na madaktari wake kuthibitisha kuwa hayuko fiti anahitaji kupumzika hivyo hatutakuwa naye,” alisema.

Alisema licha ya kukosekana kwa mshambuliaji huyo, nafasi yake haitazibwa kwani alimwita kutokana na uzoefu wake.

Mayanga alisema mchezaji pekee ambaye alikuwa hajaripoti kambini ni Farid Mussa anayecheza katika klabu ya Tenerife ya nchini Hispania, lakini aliwasili alfajiri jana.

Alisema kikosi chake kina morali ya hali ya juu na amewaomba Watanzania sapoti ili wafanye vizuri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -