Saturday, November 28, 2020

MAYANJA: MBEYA CITY WAJANJA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SALMA MPELI

KOCHA msaidizi wa Simba, Mganda Jackson Mayanja, amesema Mbeya City waliwazidi ujanja washambuliaji wao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba walibanwa katika mchezo huo  baada ya kutoka sare ya kufunga mabao 2-2 na Mbeya City,  ikiwa ni siku chache baada ya kuifunga mabao 2-0 Yanga.

Akizungumza na BINGWA juzi, Mayanja, alisema tatizo kubwa lililofanya washindwe kuibuka na ushindi ilitokana na washambuliaji wao kubanwa na kupoteza nafasi nyingi za kufunga.

Mayanja alisema pamoja na washambuliaji wake kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini walipoteza umakini kutokana na kuzidiwa ujanja na mabeki wa Mbeya City.

“Tulitengeneza nafasi nyingi lakini tulipoteza na kushindwa kupata mabao, tatizo kubwa lilikuwa kwa washambuliaji ambao walizipata nafasi lakini wakashindwa kuzitumia vema,” alisema.

Akizungumzia mchezo huo kwa ujumla, Mayanja alisema ulikuwa mgumu na wapinzani wao walijipanga vizuri na kuonyesha ushindani wa hali ya juu.

Mayanja alisema kuhusu mbio za ubingwa bado mechi zilizobaki ni nyingi na hawawezi kusema wamekata tamaa kutokana na matokeo hayo, kubwa ni kuendelea kupambana.

“Bado tupo kwenye mbio za ubingwa, ligi bado ni ndefu na wapinzani wetu  ambao ni Yanga katika mbio hizo bado wanakabiliwa na mechi ngumu kama ya Azam hivyo lolote linaweza kutokea,” alisema.

 

Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Kinna Phiri, ametoa lawama kwa mwamuzi aliyechezesha mchezo huo, Jacob Adongo kutoka Mara kwa madai aliingia uwanjani akiwa na matokeo yake.

Phiri alisema hakuridhishwa na uamuzi wake wa kuipa penalti Simba, wakati wakiwa mbele kwa mabao 2-1.

Alisema mwamuzi huyo ndio alikuwa kila kitu katika mchezo huo, lakini hilo limekuwa ni tatizo kubwa kwa ligi kuu kwani mara nyingi waamuzi wanaonekana kuingia uwanjani wakiwa wanajua kabisa ni timu gani inatakiwa kushinda.

“Hatujaridhishwa na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo wa leo (juzi), lakini yeye ndio mtu wa mwisho, ila katika ile penalti ya Simba tunataka kwenda kujiridhisha zaidi katika CD, ili tuone kama ilikuwa ni halali,” alisema Phiri.

Previous articleMTIBWA YAIZUIA YANGA
Next articleCIOABA AWAPA TANO AZAM
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -