Saturday, January 16, 2021

MAYAY ATAKA KURUDISHA HESHIMA YA SOKA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MARIAM SHABANI (TUDARCO) NA BLANDINA RAYMOND (TUDARCO)

MGOMBEA wa nafasi ya rais katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ally Mayay, amesema ameomba ridhaa ya kuongoza shirikisho hilo ili aweze kurejesha heshima ya soka ambayo kwa sasa imepotea.

Mayay ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’, alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua kampeni zake katika Ukumbi wa Ramada jijini Dar es Saalam.

Alisema endapo akipewa nafasi ya kuongoza, vipaumbele vyake ni kuhakikisha anarudisha heshima ya soka nchini kwa kuwaweka pamoja wadau watakaosaidia kuleta mawazo ya namna ya kuendesha mpira wa miguu kwa mafanikio.

“Moja ya kazi za rais wa shirikisho ni  kupokea maoni yenye lengo la kujenga kutoka kwa wadau, hivyo nitahakikisha naweka usawa ndani ya familia ya mpira.

“Pia nitaboresha mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwawezesha washiriki wake ambao ni klabu kujitegemea kupata udhamini kwani timu nyingi hazina wadhamini jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya soka,” alisema Mayay.

Uchaguzi mkuu wa TFF unatarajiwa kufanyika keshokutwa mkoani Dodoma, ambapo viongozi watakaochaguliwa ni rais, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -