Tuesday, October 27, 2020

MBAO YAREJEA KILELENI, STAND YANG’ARA

Must Read

Tshishimbi atambulishwa kuvaa uzi wa AS Vita

NA MWENDISHI WETU KIUNGO wa zamani wa timu ya  Yanga, Papy Tshishimbi, ametambulishwa katika...

Kaseja: Hatukuwa dhaifu kwa Yanga

NA ZAINAB IDDY NAHODHA wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC),  amesema  hawakuwa dhaifu...

Kaze amuibua Zahera, aionya Simba

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa zamani wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema aina...

GLORY MLAY NA WINFRIDA MTOI

TIMU ya soka ya Mbao FC imerejea kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuinyuka Tanzania Prisons bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Matokeo hayo yameiwezesha Mbao kufikisha pointi 13 baada ya kushuka dimbani mara sita, ambapo imeshinda mara nne, kupata sare moja na kufungwa mmoja, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Yanga waliojikusanyia pointi 12.

Bao pekee la ushindi kwa Mbao limefungwa na Ndaki Robert aliyefunga kwa kichwa katika dakika nne za nyongeza za kipindi cha pili.

Licha ya kupata ushindi huo, Mbao ilipoteza nafasi nyingi za mabao kutokana na ubora wa golikipa Aron Kalambo ambaye jana alionyesha  kiwango cha juu katika kuokoa michomo kadhaa ya washambuliaji wa timu hiyo.

Katika mchezo mwingine, African Lyon ilipokea kichapo nyumbani baada ya kufungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mabao ya Mtibwa yalifungwa katika dakika ya 25 kipindi cha kwanza na Jafari Kibaya baada ya kuwatoka mabeki wa Lyon kabla ya kuongeza la pili dakika ya 35.

Stand United pia iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Tshishimbi atambulishwa kuvaa uzi wa AS Vita

NA MWENDISHI WETU KIUNGO wa zamani wa timu ya  Yanga, Papy Tshishimbi, ametambulishwa katika...

Kaseja: Hatukuwa dhaifu kwa Yanga

NA ZAINAB IDDY NAHODHA wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC),  amesema  hawakuwa dhaifu mbele ya Yanga, licha ya...

Kaze amuibua Zahera, aionya Simba

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa zamani wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema aina ya mpira unaocheza kwa sasa...

Mtibwa yaitungua Azam Jamhuri, Prisons yazidi kupeta

NA GLORY MLAY TIMU ya Azam FC imepoteza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara jana baada...

KIPIGO CHA PILI MFULULIZO:Sven akalia kuti kavu Simba

Wengine benchi la ufundi watajwa, yeye alia na akina Bocco, Morrison NA WINFRIDA MTOI KOCHA Mkuu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -