Tuesday, November 24, 2020

MBAYA WA SIMBA AMTAKA BOSSOU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WINFRIDA MTOI

MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar, Mbaraka Yussuf, aliyeiua Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, amesema beki wa Yanga, Vincent Bossou, ajiandae.

Yussuf amemtaka Bossou kujiandaa kabla ya kukutana katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa mwezi ujao Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA juzi, alisema zamani alikuwa anawaogopa mabeki warefu na  wenye nguvu kama Bossou, lakini  kwa sasa anapenda kukutana nao uwanjani ili awafunge kirahisi.

Yussuf alisema awali alikuwa anapata shida anapojua mechi anayokwenda kucheza kuna mabeki wenye maumbile hayo.

Alisema siku hizi amejua udhaifu wa mabeki hao, kwani inakuwa ni rahisi kuwafunga kama alivyofanikiwa kumpita beki mrefu wa Simba, Abdi Banda.

“Hakuna beki ninayemhofia ligi kuu kwa sasa, kwani woga nilikuwa nao umenitoka na ndiyo sababu ya kufunga mabao mengi msimu huu.

“Ila zamani ilikuwa nikipangwa kucheza mechi nafikiria ni mabeki gani nakwenda kukutana nao kama ni warefu basi naweza hata kukimbia mechi,” alisema.

Alisema siku zote uwanjani unapokutana na mabeki wenye nguvu na wawe wakorofi ukiwa kama mshambuliaji inakufanya upambane na ukifunga bao linakuwa la ukweli.

Mshambuliji huyo amefunga mabao 11 katika michezo 25 ya ligi aliyocheza, sawa na Shiza Kichuya wa Simba, huku Simon Msuva wa Yanga akiongoza kwa mabao 12.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -