Sunday, October 25, 2020

MBELGIJI AINGIA MTEGONI MSIMBAZI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA SAADA SALIM

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, ameingia mtegoni baada ya viungo wake wawili, Haruna Niyonzima na Hassan Dilunga, kurejea uwanjani wakiwa katika kiwango cha juu, hali itakayomfanya Mbelgiji huyo kukuna kichwa nani kati ya hao wawili wakumweka Clatous Chama benchi.

Kiungo wa Zambia, Chama kwa kiasi kikubwa amejihakikishia namba katika kikosi cha kwanza huku Dilunga kabla ya kupata majeraha alikuwa sehemu ya timu hiyo na Niyonzima hakuonekana kwa muda mrefu.

Kurudi kwa Niyonzima na Dilunga,  kunaifanya timu hiyo kuwa na ongezeko la viungo wengi, lakini mashabiki walikuwa na hamu kubwa ya kuona ni yupi atafanikiwa kufanya vizuri zaidi.

Akizungumza na BINGWA jana, kocha wa viungo wa Simba, Adel Zrane,  alisema Niyonzima yupo tayari kucheza ni suala la Kocha Mkuu, Aussems kuamua kumtumia au kutomtumia.

“Dilunga anaendelea vizuri na mazoezi ya kujiweka sawa, lakini Niyonzima yuko vizuri zaidi, suala la kuanza litakuwa chini ya Aussems, pia kuwepo kwa wachezaji zaidi ya wawili katika nafasi moja ni changamoto kwao kuhakikisha wanajituma mazoezini ili kupata nafasi,” alisema.

Adel alisema si kwa wachezaji hao wawili, ana amini viungo waliosajiliwa ndani ya kikosi hicho wako vizuri, hivyo kila mmoja anahitaji kujituma zaidi ili kumshawishi kocha wao kumpa nafasi ndani ya kikosi cha kwanza.

“Ukiangalia Niyonzima yupo fiti na ni miongoni mwa wachezaji wetu walioitwa katika mataifa yao, pia Dilunga ameanza kurejea hivyo kila mmoja anatakiwa kujituma mazoezini ili kumshawishi kocha kumpa nafasi,” alisema.

Katika kumbukumbu za mchezo dhidi ya African Lyon, kwa aliyeona au kulisikia lile shangwe lililopigwa na mashabiki wa Simba wakati kiungo wao fundi, Niyonzima, alipopata nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza msimu huu, wataelewa.

Basi iko hivi, Niyonzima aliingia uwanjani dakika ya 83 kuchukua nafasi ya Chama katika mchezo ambao Simba walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lyon.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -