Saturday, October 31, 2020

MBELGIJI AIWEKA YANGA KIGANJANI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWAMVITA MTANDA


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems wa Ubelgiji, amesema atautumia muda wake kikamilifu kuhakikisha timu yake inaibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya Yanga ambao unatarajiwa kuchezwa Septemba 30, mwaka huu.

Akizungumza na BINGWA jana, kocha huyo wa Ubelgiji alisema muda huu wa mapumziko atautumia kikamilifu kuhakikisha kila mchezaji wake anakuwa fiti kwa ajili ya maandalizi ya mechi hiyo kwa kuwa hataki kupoteza dhidi ya mahasimu wao.

“Nitatumia muda huu kuhakikisha naweka sawa kikosi changu, naelewa mechi hizi zinavyokuwa na presha, sitakubali kuweka unyonge ndani ya kikosi changu kwa kufungwa na Yanga, lazima nitumie mbinu zangu kuihakikishia ushindi timu yangu,” alisema Aussems.

“Najua ukifungwa na mahasimu wako unapoteza matumaini, ila mimi nipo hapa kwa lengo la kuongeza matumaini, jambo kubwa ni wao kufanya kile ambacho nawaelekeza, matumaini ya kupata ushindi lazima kuwapo,” aliongeza Aussems.

Aussems alisema hana hofu na mchezaji hata mmoja wa kikosi cha Yanga, japokuwa anatambua uwezo wao, lakini anaamini kuwa kikosi chake ni bora zaidi.

Mbelgiji huyo alisema anatambua kuwa nyota wake wana vipaji na kila mmoja huwa anafanya juhudi anapokuwa uwanjani kuhakikisha timu yake inapata ushindi, hivyo anawaongezea ujuzi zaidi wa kupambana uwanjani na kuhakikisha wanafunga mabao mengi siku hiyo.

“Ushindi unaongeza nguvu kwa mchezaji na ndio maana unaona asilimia kubwa ya timu ambazo huwa zinaanza vizuri pia humaliza vizuri, hata kikosi changu pia kimeanza vizuri ndio maana najiamini kwa asilimia zote kuwafunga Yanga,” alisema Aussems.

Pia kocha huyo aliwataja Shiza Kichuya na Adam Salamba kuwa ni wachezaji hatari na kudai kwamba kama wataendelea kufuata kile anachowafundisha watafanya vizuri msimu huu na hata huko mbeleni.

“Hawa ni wachezaji ambao wakiwa uwanjani wanajua kupambana na wako makini sana, nawafundisha kulingana na upeo wao na kile wanachokifanya, hawa ni hatari sana,  wanaweza  kufanya mambo makubwa,” aliongeza Aussems.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -