Tuesday, October 27, 2020

MBELGIJI ALIA KUSALITIWA SIMBA SC

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA MWAMVITA MTANDA


Kitendo cha wachezaji sita wa simba kuenguliwa katika kikosi cha timu ya taifa, taifa stars, kutokana na utovu wa nidhamu, kimemkera mno kocha mkuu wa wekundu wa msimbazi, patrick aussems, akisema kuwa huo ni usaliti wa hali ya juu dhidi yake.

kocha mkuu wa taifa stars, emmanuel amunnike, juzi aliwaengua wachezaji hao nyota wa simba kutokana na kuchelewa kujiunga na kambi ya taifa kama alivyokuwa ameagiza na hivyo kuteua wengine wa kuchukua nafasi zao.

nyota hao walioondolewa stars ni erasto nyoni, jonas mkude, john bocco, shiza kichuya, hassan dilunga na shomari kapombe, lakini pia akiwamo kiungo wa yanga, feisal salum ‘fei toto’ ambaye naye alifanya kosa kama hilo.

akizungumza na bingwa jana, aussems alisema kuwa, mchezaji kuitwa katika timu ya taifa ni jambo la heshima na wapo wengi ambao walitamani nafasi hizo, lakini hawakufanikiwa, hivyo kitendo cha nyota wake kushindwa kutii sauti ya taifa lao, hakipaswi kuungwa mkono na yeyote yule.

“katika vitu ambavyo ninasisitiza katika kikosi changu ni nidhamu ambayo ndio uti wa mgongo wa mchezaji, inamsaidia aweze kuishi mazingira yoyote. kwa hiyo, kitendo cha kutomtii kocha wao wa timu ya taifa, ni kama wamenisaliti kile ambacho huwa nawafundisha,” alisema aussems.

aussems alisema hayupo tayari kulifumbia macho suala hilo na kwamba atahakikisha analivalia njuga suala hilo la utovu wa nidhamu ili wasije wakarudia tena.

“nitafanya mazungumzo nao kuhusiana na jambo hilo, naweza kusema walichofanya si busara, natambua ni wachezajia ambao mashabiki wanaamini uwezo wao, sasa kutokuwepo kwao ni sawa na kuwavunja moyo mashabiki,” aliongeza aussems.

bingwa lilifanya jitahada za kuwatafuta wachezaji hao ili kupata maoni yao juu ya hilo, lakini baadhi yao walizima simu kabisa, huku aliyepatikana akiwa ni mkude pekee ambaye hata hivyo, hakuwa tayari kuzungumzia sakata hilo na badala yake akasema wamezuiliwa na viongozi kuongelea suala hilo.

“siwezi kuzungumza chochote juu ya suala hilo, toka jana (juzi) viongozi wametupigia simu na kukataza kuongelea hayo mambo kwa vyombo vya habari,” alisema mkude.

kikosi cha taifa stars kimeweka kambi katika hoteli ya seascap, jijini dar es salaam tangu juzi, kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya afrika (afcon 2019) dhidi ya uganda, septemba 8, mwaka huu jijini kampala.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -