Monday, October 26, 2020

MBELGIJI AMKABIDHI TIMU DJUMA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

Kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, ameonekana kufanyia kazi faili la msaidizi wake, Masoud Djuma ambaye alimpa kazi ya kukisoma kikosi cha Yanga kilipovaana na Coastal Union na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa, michezo iliyopigwa ndani ya wiki iliyopita.

Djuma alibaki Dar es Salaam kuisoma Yanga wakati kikosi chao kiliposafiri kwenda Mtwara kucheza na Ndanda kabla ya kuzifuata Mbao FC ya Mwanza na Mwadui ya Shinyanga.

Kwa kifupi, yeyote anaweza kusema kuwa Djuma ndiye aliyekabidhiwa kikosi cha Simba, kwani mbinu, mifumo na ufundi watakaoutumia kesho utategemea na ripoti yake jinsi alivyowasoma Yanga.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinadai kuwa baada ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao kuwasili Dar es Salaam kutoka Shinyanga, Djuma alijifungia na Aussems na kumweleza yale aliyoyaona Yanga kuona ni jinsi gani wanayafanyia kazi.

Pamoja na mambo mengine, habari zinadai kuwa ripoti ya Djuma inaelezea jinsi Yanga walivyo hatari katika safu ya ushambuliaji, huku ukuta wao ukiwa si imara sana.

Kutokana na taarifa hizo, katika mazoezi ya jana ya Simba yaliyofanyika Uwanja wa Gymkhana, jijini, Aussems alikuwa akiwakomalia washambuliaji wake wakiongozwa na Meddie Kagere na Emmanuel Okwi, kuhakikisha wanamaliza kazi mapema.

Mbali na safu hiyo ya ushambuliaji, pia Aussems alikuwa akiwasuka kikamilifu mabeki wake, Pascal Wawa, Erasto Nyoni na Jjuuko Murushid kutofanya makosa.

Mmoja wa vigogo wa Simba aliliambia BINGWA jana akisema: “Tunachokitaka ni kuhakikisha tunamaliza mchezo mapema na kuwarudisha mashabiki wetu majumbani mwao wakiwa wamejawa na furaha.”

Kwa upande wake, Kocha wa viungo wa timu hiyo, raia wa Tunisia, Adel Zrane, alisisitiza: “Wachezaji wote wapo vizuri na yeyote anaweza kucheza na kufanya vizuri kutokana na kuwa timamu kimwili na akili.”

Previous articleWATAJIBEBA
Next articleYANGA WATEGUA MITEGO
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -