Tuesday, October 27, 2020

MBELGIJI AMPELEKA DJUMA YANGA

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA SAADA SALIM


WAKATI wapenzi wa soka nchini wakiwa wamepigwa na butwaa kutokana na kitendo cha Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, kubaki Dar es Salaam wakati kikosi chao kikiwa Mtwara, imefahamika Yanga ndiyo iliyomzuia Mrundi huyo kuwaona vijana wake wakivaana na Ndanda FC leo.

Simba na Ndanda zitashuka kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona leo kuonyeshana kazi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Wekundu wa Msimbazi wakiwa wamepania kuzoa pointi zote tatu.

Lakini benchi la ufundi la Simba litaongozwa na kocha mkuu pekee, Mbelgiji Patrick Aussems, huku Djuma akiwa na kazi maalumu iliyombakiza jijini Dar es Salaam.

Habari zilizolifikia BINGWA juzi, zinasema kuwa Djuma amebaki Dar es Salaam kwa kazi maalumu ambayo ni kufuatilia michezo ya watani wao wa jadi, Yanga watakaovaana na Stand United kesho kwenye Uwanja wa Taifa.

Aussems anafahamu kuwa pamoja na ubora wa kikosi chake, lakini kuifunga Yanga kuna maana kubwa kwake na timu yake kwa ujumla kuelekea safari yake ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na kufanya kweli kimataifa.

Ni kutokana na hilo, ameona ni vema Djuma akabaki Dar es Salaam ili kuisoma vizuri Yanga hivyo atakapokutana naye, wajue ni vipi wanakabiliana na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara wa kihistoria.

Lakini alipoulizwa juu ya kubaki Dar es Salaam kwa Djuma, Aussems alizuga akidai kuwa kocha mwenzake huyo ana programu maalumu ya kuwanoa wachezaji waliosalia jijini.

Juzi na jana asubuhi, Djuma aliendelea na programu ya mazoezi ya wachezaji wao waliobaki jijini kwenye Uwanja wa Kinesi, uliopo Urafiki ambao waliongezewa nguvu na baadhi kutoka kikosi cha vijana, yaani Simba B.

Wachezaji wa kikosi cha kwanza waliohudhuria mazoezi hayo ni kipa Ally Salim, Mohammed Rashid, Yusuph Mlipili, Abdul Selemani na Hassan Dilunga, aliyekuwa majeruhi.

Taarifa kutoka ndani ya Simba, zinasema kwamba mbali ya kuwapeleleza Yanga, Djuma pia ‘ataipiga chabo’ mechi kati ya African Lyon na Coastal Union itakayopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

“Hakuna tatizo lolote, ila ni mgawanyo wa majukumu tu, ukizingatia kuna mechi zinaendelea hapa jijini, hivyo kocha mkuu ameliangalia na kumtaka msaidizi wake kuendelea na programu kwa wachezaji waliobakia Dar es Salaam pamoja na kufuatilia wapinzani wetu katika michezo itakayoendelea,” alisema kiongozi mmoja wa Simba.

Alisema Aussems anataka kuhakikisha wamewasoma vilivyo Yanga kabla ya kukutana nao Septemba 30, mwaka huu katika mchezo wa kwanza Ligi Kuu Bara.

“Kwa sasa timu zote zimejiandaa vyema, kwa kuwa Aussems ameambata na kocha wa viungo, Adel Zrane, huku Dar es Salaam, Djuma ataendelea na majukumu ikiwemo kuwasoma wapinzani wetu, hasa mchezo wetu dhidi ya Yanga,” alisema mtoa habari wetu huyo.

Kwa upande wake, Djuma, alisema: “Kubaki Dar es Salaam ni kutokana na mgawanyo wa majukumu, nitahakikisha tunafanya kazi nzuri kwa kuendelea na majukumu aliyonipa (Aussems) kuhakikisha tunafanya vyema katika michezo iliyobakia.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -