Wednesday, October 28, 2020

MBELGIJI APIGA MKWARA SIMBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WAANDISHI WETU


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amekisikia kilio cha mashabiki wa timu hiyo kufanyia kazi safu yake ya ushambulizi kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi wanazopata kwa kupata mabao mengi zaidi ya msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Msimu uliopita ulikuwa wenye mafanikio kwa Emmanuel Okwi, baada ya kumaliza ligi akiwa mfungaji bora, akipachika mabao 20, akifuatiwa na Bocco (14), sawa na Marcel Kaheza aliyekuwa akitumikia Majimaji na sasa yupo ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao.

Okwi na Bocco ndiyo kombinesheni iliyofanya vizuri zaidi msimu huo, baada ya kufunga mabao 34 kati ya 62 yaliyowekwa kimiani na kikosi cha timu hiyo.

Kitendo cha Simba kusajili wachezaji wanaoamini ni wa kiwango cha juu, lakini pia kuweka kambi Uturuki, kiliwafanya mashabiki wa timu hiyo kuamini timu yoyote watakayokutana nayo wataishushia mvua ya mabao.

Lakini kwa kuanza ligi na ushindi kiduchu, hali hiyo imeonekana kuwashtua watu wa Simba, wakihoji kulikoni!

Akizungumza na BINGWA Dar es Salaam jana, Aussems alisema anaendelea kukinoa kikosi chake, hasa safu yake ya ushambuliaji kwa kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza, ili kuibuka na ushindi mnono katika mchezo ujao.

“Bado sijaridhishwa na kiwango cha timu yangu, hasa katika safu ya ushambuliaji, naendelea kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza huku nikiendelea kuimarisha kwa kuwapa majukumu mastraika wangu kwa kufikia malengo tuliyojiwekea kwa msimu huu.

“Ukiangalia katika mchezo wetu na Prisons tulikosa nafasi nyingi za wazi, hivyo hilo nimeliona na kuhakikisha nalifanyia kazi, kwani kila mchezaji anajua majukumu yake na sasa ni kuyatekeleza,” alisema.

Aussems alisema katika mechi iliyopita, alikosekana Okwi kutokana na kupata majeraha katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar, ambapo kwa sasa yupo katika matibabu na anaamini siku mbili hizi itakuwa habari nzuri kwa mshabiki kutarajia kuonekana katika mchezo dhidi ya Mbeya City.

Kikosi cha Simba kiliendelea na mazoezi juzi na jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mbeya City, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Jumatatu wiki ijayo.

IMEANDALIWA NA SAADA SALIM, DEBORA MBWILO (TUDARCO) NA NICE GODFREY (DSJ)

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -