Sunday, October 25, 2020

MBELGIJI AWAKOMALIA KICHUYA, SALAMBA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA SAADA SALIM

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, ameendelea kuumiza kichwa kutokana na washambuliaji wa timu hiyo kushindwa kufunga mabao mengi katika michezo saba ya Ligi Kuu Tanzania Bara waliyocheza hadi sasa.

Mpaka sasa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu wamefanikiwa kupachika mabao nane pekee, idadi ambayo imemfanya kocha huyo raia wa Ubelgiji kuanza kuifanyia kazi safu ya ushambuliaji kabla ya kuvaana na Stand United.

Katika kuhakikisha anamaliza tatizo la umaliziaji, Mbelgiji huyo ameanza kuwasimamia vilivyo; Adam Salamba, Shiza Kichuya, Mohamed Rashid, Mohamed Ibrahim na Marcel Kaheza, kwa kila hatua ili waweze kubadilika na kuendana na kasi ya kufunga mabao.

Mpaka sasa ni wachezaji wanne waliofanikiwa kufunga mabao ndani ya kikosi hicho cha Msimbazi ambao ni Meddie Kagere (manne), John Bocco (mawili) pamoja na Emmanuel Okwi na Kichuya waliofunga bao moja moja.

Aussems ameuahidi uongozi kuwa atatumia wiki mbili za mapumziko kuboresha kikosi na kuwapa mbinu wachezaji, hasa katika safu ya ushambuliaji ili kuondokana na changamoto ya kupata idadi ndogo ya mabao kama ilivyokuwa kwa michezo iliyopita.

Akizungumza na BINGWA jana, Aussems alisema wachezaji wanatengeneza nafasi nyingi lakini wanashindwa kuzitumia, hali inayofanya mashabiki kumjia juu na kuingiwa na hofu juu ya mwenendo wa timu hiyo katika mbio za kutetea ubingwa.

Alisema hajafurahishwa na kasi ya upachikaji mabao wakati Simba ina kikosi kipana chenye  wachezaji bora ambao wanahitaji kuongezewa ujuzi tu ili wafanye vizuri zaidi.

“Tuna wachezaji wengi wazuri ambao wanahitaji kupewa ujuzi zaidi hasa wa kuzitumia nafasi wanazozipata katika mashindano tunayoshiriki, ninaamini baada ya kukaa nao wiki mbili kikosi kitakuwa vizuri,” alisema.

Aidha, alisema anaamini muda huo unatosha  kujenga kikosi bora kitakachotetea taji la ubingwa na kikubwa atahakikisha wachezaji wote wanakuwa makini katika majukumu anayowapa mazoezini.

“Safu ya ushambuliaji ina wachezaji wengi wazuri ambao wanaweza kufanya mambo makubwa kwa timu ila ni jambo la kusubiri tu ili waweze kuwa katika ubora wao,” alisema Aussems.

Kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani, ambapo Aussems ameonekana kuwa mkali kwa wachezaji waliopo kikosini akiamini wanaweza kubadilika taratibu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -