Sunday, November 1, 2020

MBELGIJI: MBEYA CITY HAWATOKI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWAMVITA MTANDA


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuibuka na ushindi katika mechi ya leo dhidi ya Mbeya City, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa.

Akizungumza na BINGWA jana, Aussems, alisema tayari amerekebisha makosa ya kikosi chake ambayo  yaliwafanya washindwe kuibuka na ushindi wa mabao mengi katika mechi iliyopita.

Aussems alisema katika mchezo huo wa kwanza kikosi chake kilikuwa na nafasi ya kufunga mabao mengi, lakini kilichowakwamisha ni kutozoea mfumo mpya na kubadilisha safu ya ushambuliaji.

“Sina sababu ya kuwa na hofu ya kikosi changu, mimi ni mwalimu mzoefu, kama tulifanikiwa mechi iliyopita hata hii uhakika upo, tufafunga mabao mengi kwa kuwa nimesharekebisha makosa yote yaliyofanya tukose mabao ya kutosha mechi ya kwanza,” alisema Aussems.

Aidha, Mbelgiji huyo alisema yupo hapa nchini kwa lengo la kuisaidia Simba, hivyo atatumia uzoefu wake kuhakikisha  wanashinda michezo mingi ili wafanikiwe kutetea ubingwa wao.

Aussems alisema itakuwa ni faraja kwake kuona timu yake inafunga mabao mengi katika mechi ya leo, baada ya kurekebisha safu ya ushambuliaji ambayo ilikuwa kikwazo mechi ya kwanza.

“Bado tuna safari ndefu, tukicheza kesho (leo) tutabakisha mechi nyingine 16 za mzunguko wa kwanza, hivyo lazima tupambane sana ili kupata ushindi na lengo letu ni kufanya vizuri katika michezo hii ya awali,” aliongeza Aussems.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -