Wednesday, October 21, 2020

MBELGIJI: SALAMBA ANA KAZI MAALUM

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA MWAMVITA MTANDA


MASHABIKI wa Simba wametolewa wasiwasi juu ya hatima ya mshambuliaji wao, Adam Salamba, wanayetamani kumwona akifanya mambo kikosini mwao kwa kuambiwa kuwa mkali huyo aliyetokea Lipuli ya Iringa ana kazi maalumu.
Salamba ni miongoni mwa wachezaji wapya wa Simba waliotua Msimbazi mwishoni mwa msimu uliopita, akiwa ameitumikia vema timu yake hiyo mpya kwa kufunga mabao matano katika mechi za michuano ya Kombe la Kagame na za kirafiki nchini Uturuki.
Kutokana na makali yake hayo, Salamba alikuwa akitajwa kama mchezaji mwenye uwezo wa kuibeba Simba katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, sambamba na nyota wengine wapya kama Meddie Kagere, Hassan Dilunga, Cletus Chama, Pascal Wawa na wengineo.
Lakini straika huyo hadi sasa hajacheza mechi yoyote kati ya mbili za Ligi Kuu Bara ambazo timu yake imecheza na kushinda zote dhidi ya Tanzania Prisons (1-0) na Mbeya City (2-0).
Badala yake, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amekuwa akiwatumia John Bocco na Kagere kama washambuliaji wa kati, huku nyuma yao kukiwa na viungo, Dilunga, Shiza Kichuya, James Kotei, Muzamir Yassin na Said Ndemla.
Akizungumza na BINGWA jana juu ya kitendo cha kumweka benchi Salamba, Aussems, alisema kulingana na mfumo wake, anakuwa na utaratibu wa kuwapanga washambuliaji wake kutokana na mechi husika.
Aussems alisema Salamba ni mchezaji mwenye kipaji na makini anapokuwa uwanjani, hivyo kwa kuwa tayari alishapangwa katika mechi kadhaa zilizopita, kwa sasa amempa kazi maalumu ya kukusanya nguvu tayari kuipigania timu yake hiyo katika mechi zinazohitaji mshambuliaji wa aina yake.
“Salamba kiwango chake ni bora, amecheza mechi nyingi na amefanikiwa kufunga mabao, sioni sababu ya kumpanga kikosi cha kwanza kila mechi, naweza kumchosha mapema, mchezaji mzuri hupewa nafasi ya kupumzika ili mwili ukae fiti.
“Kwa muda mfupi ambao nimekuwa naye (Salamba), nimeweza kumtambua kuwa ni mchezaji ambaye ana kiu ya kufanya vizuri na huwa anajituma sana akiwa uwanjani kuhakikisha anaisaidia timu yake kwa kufunga mabao. Nina imani nitakapompanga tena, atafanya vizuri zaidi,” alisisitiza Mbelgiji huyo.
Aussems, alisema kutokana na uzoefu wake katika soka, anapoanza kukinoa kikosi kipya, huwa anasoma tabia na uwezo wa kila mchezaji hali ambayo inamsaidia jinsi ya kuwapanga, jambo ambalo tayari ameshalifanya kwa mchezaji huyo.
Aussems alisema kwa kuwa umri wa mshambuliaji huyo bado mdogo, anayo nafasi kubwa ya kuendelea kufanya vizuri na kuibeba mno Simba.
BINGWA lilimtafuta Salamba kupata maoni yake juu ya kitendo cha kusotea benchi ambapo alisema hana hofu na hilo akiamini hali hiyo inamsaidia kujifunza kile ambacho wenzake wanakifanya uwanjani na kurekebisha makosa yake.
“Kikosi chetu kina wachezaji wazuri tena wakongwe ambao nimewakuta, hivyo sina hofu na hilo, kwa kuwa najifunza kutoka kwao, ila natambua uwezo wangu hata nikipangwa kila siku ninaweza kufanya vizuri,” alisema Salamba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -