Friday, October 30, 2020

MBELGIJI: SIWAHOFII YANGA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWAMVITA MTANDA


 

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Mbelgiji Patrick Aussems, amesema kwamba hana shaka yoyote juu ya pambano la watani wa jadi dhidi ya mahasimu wao Yanga litakalopigwa Septemba 30, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mpaka sasa Simba tayari imeshuka dimbani mara tano katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara na kufanikiwa kufunga mabao sita, ambapo imeshinda michezo mitatu, kupata sare moja na kufungwa mmoja, hivyo kufikisha pointi 10.

Akizungumza na BINGWA jana, Aussems, alisema hana wasiwasi na mechi hiyo ambapo sasa anakisuka vyema kikosi hicho tayari kwa kukabiliana katika mtanange huo.

“Natambua hii ni mechi ngumu lakini tumejipanga kwa matokeo chanya, kwa sasa naandaa kikosi kikamilifu ili kiweze kupambana, pia ninaamini tutafanikiwa kuibuka na ushindi,” alisema Aussems.

Aussems aliongeza kuwa hii ni mara yake ya kwanza kukutana na Yanga tangu alipoanza kukinoa kikosi hicho cha Msimbazi katika Ligi Kuu msimu huu, lakini anaamini hakuna jambo jipya litakalowatisha kwani tayari ameshaangalia baadhi ya mechi zao kupitia video.

“Sioni kama kuna jambo ambalo litawasumbua wachezaji wangu, nimeshaangalia mechi zao zilizopita na nawajua mastraika wao, nitapanga kikosi kikamilifu ili tuwasumbue kama msimu uliopita ambao mimi sikuwepo,” alisema Aussems.

Kikosi cha Simba kilitua Dar es Salaam juzi usiku kikitokea jijini Mwanza, ambako kilicheza mechi dhidi ya Mbao FC na kufungwa bao 1-0 kabla ya kuifuata Mwadui FC mkoani Shinyanga na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Kwa mujibu wa Mkuu Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, sasa  wanafanya mikakati wa kuiweka kambini timu hiyo ili kujiandaa na pambano hilo la Jumapili dhidi ya mahasimu wao Yanga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -