Sunday, October 25, 2020

MBEYA CITY WATAMBA KUMSHANGAZA MO DEWJI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA SALMA MPELI


WAKATI Simba wakitamba kuwa leo wataibuka na ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, wapinzani wao Mbeya City FC wamejibu mapigo.

Mbeya City wameahidi kuwashangaza Wekundu hao wa Msimbazi mbele ya bosi wao mfanyabiashara, Mohamed Dewji ‘Mo’.

Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Habari wa timu hiyo, Shaha Mjanja, alisema hawakuja Dar es Salaam kufungwa, hivyo leo wataiwashia moto Simba.

Alisema kufungwa ni sehemu ya mchezo lakini wiki iliyopita walifungwa na Azam FC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, hivyo watahakikisha wanaondoka na pointi kwenye mchezo huo dhidi ya Simba.

“Tumejiandaa kushinda, hatukuja Dar kupoteza na ikitokea kufungwa ni sehemu ya mchezo, lakini hayo si matarajio yetu kwani tungejua kama tutafungwa tusingefanya maandalizi,” alisema Mjanja.

Mjanja aliongeza kuwa wanafahamu uwezo wa Simba na nguvu ya kikosi chao, lakini hilo haliwatishi kwani anaamini maandalizi yao yatawasaidia kuondoka na pointi tatu.

Alisema kuifunga Simba wakiwa nyumbani ni rahisi kwani msimu wa 2015/16 walifanya hivyo kwa kuwachapa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa.

Mbali na mchezo huo, leo kutakuwa na michezo mingine ya Ligi Kuu ambapo Azam FC itawakaribisha Ndanda FC, huku Alliance ikiwa wenyeji wa African Lyon ya Dar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -