Tuesday, November 24, 2020

Mchanganuo udhamini DTB upo wapi?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ESTHER GEORGE

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeingia udhamini na Diamond Trust  Benki (DTB), kwa lengo la kuboresha ushindani wa  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

DTB wamekuwa ni sehemu ya wadhamini wakuu wa ligi hiyo pamoja na Kampuni ya Simu ya Mikononi ya Vodacom Tanzania, ambao wamesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Sh milioni 250 na shirikisho hilo.

Mkataba huo umekuja baada ya Kampuni ya Azam Media kuingia mkataba mnono na TFF wa kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Bara.

Azam wamesaini mkataba wa Sh bilioni 23 kwa miaka mitano na sehemu ya mkataba huo uliofanyiwa marekebisho mwaka huu, ambapo klabu zinashiriki ligi hiyo zinapata Sh milioni 126 kwa mwaka.

Sehemu nyingine za fedha hizo zimekwenda Bodi ya Ligi na TFF kwa ajili  ya  masuala ya utawala.

Lakini mkataba wa Vodacom kwa TFF  unasaidia kupunguza baadhi ya gharama za uendeshaji wa klabu, kwani unafuu wanaopata ni timu kuweza kupata fedha kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya unapoanza hadi kumpata bingwa.

Kutokana na mkataba huo, klabu zinapata angalau kusafiri hadi kituo cha mchezo, ingawa fedha wanazopewa kupitia udhamini wa Vodacom hazitoshi kulingana na gharama ya uendeshaji wa timu hizo.

Pamoja na Vodacom kutoa vifaa, zawadi ya ubingwa, nauli, lakini bado mzigo umekuwa ni mkubwa kwa klabu, hasa kwa zile ambazo zinategemea udhamini wa Vodacom.

Timu zimekuwa katika wakati mgumu wa kucheza soka la ushindani kutokana na baadhi ya klabu kukabiliwa na ukata mkubwa na kujikuta zikipanda na kushuka baada ya kushiriki msimu mmoja.

Kutokana na udhamini unaoweza kukidhi mahitaji ya klabu hiyo, kunaifanya shirikisho la soka kujaribu kutafuta wadhamini wengine ambao wataweza kusaidia na Vodacom ili kuiwezesha ligi kuwa na ushindani mkali.

Jumanne wiki hii, familia ya soka imeshuhudia TFF wakipata udhamini wa mwaka mmoja kutoka kwa DTB, ambayo imeungana na Vodacom kuwekeza sehemu ya faida yao kwenye soka.

Uamuzi wa DTB kuungana na wadhamini wakuu wa ligi hiyo kuungana na wadhamini wengine kuwekeza katika soka ni jambo zuri, kwa kuwa baadhi ya wateja wao ni jamii ya wapenda kandanda.

Lakini tukiangalia kwa jicho jingine, udhamini wa DTB ni wa kitoto, kwa wao kutoa kiasi kidogo kama hicho, fedha ambazo zinaweza kutolewa na mchezaji mmoja wa Yanga, kama Obrey Chirwa.

Tuseme kwamba Chirwa anaweza kuungana na Vodacom, Azam kudhamini Ligi Kuu Bara kama usajili  na mshahara wake  unakaribia kufikia Sh milioni 250, ambazo DTB wametoa katika udhamini wao.

DTB wametoa udhamini huo, lakini ukifanya mchanganua wa fedha hizo, kila timu inaweza kupata Sh milioni 12.5 ambacho ni kiwango kidogo sana.

Timu kama Simba na Yanga, zinatumia zaidi ya Sh milioni 15 katika maandalizi ya mechi moja, huku Majimaji ikisafiri kutoka Songea mpaka Bukoba mkoani Kagera, inaweza kutumia zaidi ya fedha hizo ambazo mchanganuo wake haujawekwa hadharani kama ule wa Vodacom na Azam Media.

Mchanganua wa mkataba wa udhamini wa DTB upo wapi ili wadau wa soka waweze kujua klabu zitanufaika vipi na sehemu ya mkataba huo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -