Friday, November 27, 2020

MECHI 164, KUFUNGWA 18 BARCA WAMEMCHOKA LUIS ENRIQUE!

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

GERALD Pique huenda akawa ameongea maneno machache yaliyobeba maneno mengi kwenye kifua cha Luis Enrique, wakati huu.

“Tulikuwa ovyo kabla hajaja na baadaye tukabeba mataji matatu ndani ya msimu mmoja,” ilikuwa kauli ya Pique baada ya Luis Enrique kutangaza hadharani kuwa hataifundisha tena Barcelona msimu ujao.

Enrique aliingia Barca mwaka 2014 akichukua nafasi ya Tata Martino, amekuwa kocha wa kwanza ndani ya Camp Nou kubeba mataji 10 ndani ya misimu mitatu, ajabu sasa anaonekana si lolote.

Pique yuko sahihi sana, Enrique aliikuta Barca iliyopoteza dira zaidi ya ilivyo sasa lakini alitulia na kuibadilisha kwa kasi iliyowarudisha Wakatalunya hao kuendelea na ubabe wao wa soka duniani.

Amebakisha miezi mitatu kabla ya kuondoka Camp Nou, lakini bado yuko kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, Barca iko kileleni mwa La Liga na watacheza fainali ya Kombe la Mfalme, hivi ndivyo Enrique anavyoiacha Barcelona.

Zipo lawama kuwa Enrique amebadilisha falsafa za klabu hiyo kwa kucheza soka kumiliki mpira, chini yake Barca wanacheza soka la kushambulia na wakati mwingine kutumia sana mashambulizi ya kushtukiza ‘Counter attack’.

Lakini Barca wameanza kumlaumu Enrique na kusahau kuwa kosa la kwanza lipo kwa uongozi wao kwa kushindwa kupata mtu sahihi wa kuziba pengo la Xavi. Nani amerithi viatu vya Xavi pale Camp Nou?

Lakini si kwamba Barca wamempoteza Xavi tu msimu huu, hawana mtu aliyerithi viatu vya Dani Alves aliyetimkia Juventus na bado ni shida kwao kucheza pindi Andres Iniesta anapokuwa.

Bila kuwa na Iniesta aliye katika ubora wake, Xavi na Dani Alves ni ngumu kuiona Barca ikiwa na taswira aliyoiacha Pep Guardiola.

Kosa jingine lililofanywa na Barca ni kumuuza Thiago Alcantara, unategemea Enrique aendelee kucheza soka la kumiliki mpira kwa viungo wapi?

Na ni uendawazimu kwa kucheza soka la kumiliki mpira wakati safu yako ya ushambuliaji ikiwa na Neymar Jr, Luis Suarez na Lionel Messi.

Kweli alifeli katika Jiji la Paris, lakini yatupasa kukumbuka kuwa ni mfumo huu wa Enrique uliofanya kazi kule Berlin na kuipa Barca taji ya Ligi ya Mabingwa, wakiichapa Juventus.

Barca watamkumbuka sana Enrique, si rahisi kwa kocha kupata mafanikio kama yake kwenye msimu wake wa kwanza.

Japo alianza maisha kwa misukosuko mingi pindi alipomweka benchi Lionel Messi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Real Sociedad.

Barca walipoteza pambano hilo kwa kichapo cha bao 1-0, ghafla siku inayofuata Messi akagoma kwenda mazoezini na hapo lawama zikaanza kuelekezwa kwa Enrique.

Unajua ni kwanini Messi hakupangwa dhidi ya Real Sociedad? Siku moja kabla ya mechi wakiwa mazoezini, Messi alikwatuliwa kwenye eneo la hatari na mwenzake lakini Enrique aliyeshika filimbi akapeta, Leo akanuna!

Huu ndio ugumu wa kuishi Camp Nou kama kocha huku timu nzima kuanzia uongozi mpaka mashabiki wakielekeza mapenzi yao kwa Mfalme, Lionel Messi.

Lakini pamoja na changamoto hizo, Enrique alirudi nyuma na kutulia na baadaye kubeba mataji makubwa matatu kwa msimu.

Miezi mitatu iliyobaki ndio itakayoamua namna ya kuizika historia yake ndani ya Camp Nou, akumbukwe kama mfalme au asahaulike milele.

Akifanikiwa kufanya maajabu ya kuwatoa PSG, kubeba La Liga na kutwaa Kombe la Mfalme, ni hakika kuwa siku atakayoondoka kila chozi litamwagwa kumuaga, lakini mambo yakienda kinyume, rekodi zote za Enrique zitazima milele.

Takwimu za Enrique akiwa na Barca

Alikabidhiwa timu, Julai 2014

Mechi: 164

Ushindi: 125

Sare: 21

Kufungwa: 18

Wastani wa ushindi: 76.2%

Mataji: La Liga (2015, 2016), Copa del Rey (2015, 2016), Kombe la Ligi (2016), Ligi ya mabingwa (2015), UEFA Super Cup (2015), Klabu bingwa ya dunia (2015)

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -