Wednesday, October 28, 2020

MECHI YAKE YA 100 YAMLETEA BALAA FELLAINI 

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LIVERPOOL, England


MASHABIKI wa soka wa Manchester United wameonyesha hasira zao kupitia mtandao wa kijamii wa twitter, kwa kumlaumu kiungo mkabaji, Marouane Fellaini, aliyeingia kipindi cha pili dhidi ya Everton katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa juzi.

Muda mfupi baada ya kuingia uwanjani kutokana na mabadiliko yaliyofanywa na kocha, Jose Mourinho, Fellaini alisababisha adhabu ya penati iliyopigwa na Leighton Baines na kuisawazishia timu yake katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Kupitia mtandao huo, baadhi  ya mashabiki kwa kejeli walimpongeza kiungo huyo wa Ubelgiji kwa kufikisha mchezo wake wa 100 katika Ligi, huku wengine wakiutaka uongozi kumuuza.

Nafasi katika kikosi cha kwanza imekuwa finyu kwa kiungo huyo mkabaji, baada ya wachezaji wenzake,  Henrikh Mkhitarayan na Anthony Martial kung’ara na mashabiki wengi wanadhani mwisho wa Fellaini ndani ya klabu hiyo umefika.

Alikuwa mchezaji muhimu kwa aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Van Gaal na baada ya kuajiriwa kwa kocha, Jose Mourinho, alisema anampa Fellaini  ‘mapenzi’ anayostahili.

Mourinho  alimpanga Fellaini katika mechi kadhaa, lakini Mreno huyo aligundua kuwa angepoteza mashabiki wengi iwapo angeendelea kumpanga.

Jana kocha huyo alitetea uamuzi wake wa kumuingiza Fellain ili kupunguza kasi ya Everton na mchezo wao wa kutumia nguvu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -