Wednesday, October 28, 2020

MEDALI OLIMPIKI 2020 SI TIBA YA UGONJWA RIADHA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

KWA kipindi kirefu, mchezo wa riadha hapa nchini umekuwa taabani. Imekuwa ni kawaida kwa wawakilishi wetu kwenye michuano ya kimataifa kurudi mikono mitupu.

Yapo mengi yamekuwa yakitajwa kuwa sababu ya mchezo huo kuwa kwenye hali mbaya, ikiwamo maandalizi duni.

Mara nyingi wanariadha wa Tanzania wamekuwa na  maandalizi ya kulipua, yasiyoendana na ushindani uliopo kwenye mashindano ya kimataifa.

Hivi karibuni, Shirikisho la Riadha hapa nchini (RT) lilifanya uchaguzi mkuu wake ambapo tulishuhudia uongozi mpya ukiingia madarakani.

Moja kati ya matumaini ya wadau wengi wa riadha ni kuona ‘RT mpya’ ikiufufua mchezo huo, ndicho tunachokiamini.

Hata hivyo, bado nimebaki na maswali baada ya kuisikia kauli ya Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Wilhelm Gidabuday.

Gidabuday alisema RT itahakikisha wanariadha wa Tanzania wanarudi na medali katika michuano ya Olimpiki ya mwaka 2020 itakayofanyika jijini Tokyo, Japan.

Si mbaya, ni wazo zuri, hasa ikizingatiwa kuwa wadau wa riadha hapa nchini wamechoshwa na utamaduni wa wanamichezo wao kuwa wasindikizaji kwenye mashindano ya kimataifa.

Lakini je, ni wakati sahihi kwa Tanzania kupigia hesabu medali za Tokyo?

Ikiwa imebaki takribani miaka mitatu pekee kabla ya kuanza kwa mashindano hayo, hali ya mchezo wa riadha hapa Bongo inaridhisha kiasi kwamba tunaanza kuziota medali?

Sikatai kuwa tunaweza kuambulia japo medali moja, lakini shaka yangu ni kwamba huenda ikawa ni kwa kubahatisha zaidi.

Ninachokimaanisha ni kwamba, tumefika mbali sana kufikiria medali kwa hali iliyopo sasa kwenye riadha. Kwa tathmini ya haraka, hiyo inaweza kutuchukua hata zaidi ya miaka 10.

Kuufanya mchezo wa riadha kufikia ‘levo’ za wenzetu Kenya, Ethiopia na Jamaica, si jambo la kipindi kifupi namna hiyo.

Bado changamoto za mchezo wa riadha ni nyingi mno na zinatakiwa kutolewa macho na si kuanza kuziweka akilini medali za Tokyo.

Hivi sasa, riadha si miongoni mwa michezo inayopewa nafasi kubwa shuleni, ikimaanisha kuwa mwamko ni mdogo katika ngazi za chini. Mbali na hilo, idadi ya viwanja vyenye ubora wa kimataifa ni tatizo sugu.

Kama changamoto hizo zitafanyiwa kazi, basi mchezo wa riadha hapa nchini utakuwa umepiga hatua kuliko kushinda medali 10 za Tokyo bila mipango thabiti.

Lakini pia, kutokana na uwepo wa miundombinu inayosapoti maendeleo ya mchezo huo, kutakuwa na mwendelezo wa mafanikio ya wanamichezo wetu kwenye michuano ya kimataifa.

Yaani kama Tanzania itapata medali mwaka 2020 ikiwa na matatizo hayo, basi hatutakuwa na imani ya kuvuna nyingine ifikapo mwaka 2014.

Hapo tutakuwa tukitegemea bahati na si mipango thabiti inayoweza kutumiwa na mwanariadha yeyote wa Tanzania kushinda medali.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -