Friday, December 4, 2020

MEJA MINGANGE NDANDA ISIKUFIE MIKONONI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ONESMO KAPINGA

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea Jumamosi hii baada ya kusimama kwa muda kupisha michuano ya kimataifa.

Mechi zitakazochezwa siku hiyo ni mabingwa watetezi Yanga na Azam kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Ni mechi ngumu kwani Yanga wanaoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 53, watahitaji ushindi dhidi ya Azam ili waweze kuishusha Simba kileleni na wao kujiweka katika mazingira bora zaidi ya kutetea ubingwa wao.

Azam wao wanaoshika nafasi ya tatu kutokana na pointi 44, hawatakubali kufungwa kirahisi kama ambavyo wametoka kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Kutokana na mazingira ya mechi hiyo, Azam watakuwa na shauku ya kutaka kushinda ili kulinda heshima yao, lakini Yanga watakuwa na presha ya kutaka kupata matokeo mazuri hasa ukizingatia walifungwa na Azam kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kule Zanzibar.

Mechi nyingine itakayopigwa Jumamosi hii ni kati ya Mbeya City na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Sokoine, ambapo timu hizo zitasaka ushindi ili ziweze kujiweka katika mazingira bora zaidi katika msimamo wa ligi hiyo.

Lakini ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa Kagera Sugar kucheza na Simba kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

Ni mechi ngumu kwani Kagera Sugar hawatakubali kufungwa kirahisi, baada ya kutolewa na Mbao katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) kwa kufungwa mabao 2-1 kwenye uwanja wao huo wa nyumbani.

Pamoja na kuwepo kwa mazingira hayo, Simba watakuwa na kibarua kimoja cha kuhakikisha wanashinda ili waweze kuendelea kukaa kileleni wenye pointi 55 baada ya kucheza mechi 24.

Wenyeji Tanzania Prisons watavaana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Sokoine na Majimaji watavaana na African Lyon kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Majimaji watakuwa na wakati mgumu wa kuhakikisha wanashinda dhidi ya African Lyon, ili waweze kujinasua na mstari mwekundu wa kushuka daraja msimu huu.

Timu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya 15 kutokana na pointi 22 baada ya kucheza mechi 24 sawa na African Lyon yenye pointi 26.

Kutokana na matokeo hayo, Majimaji watatakiwa kushinda mechi zao zote zilizobaki huku ikiomba timu nyingine kama JKT Ruvu inayoshika mkia kwenye msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 20, kuendelea kufanya vibaya.

JKT Ruvu inawezekana ikawa timu ya kwanza kushuka daraka msimu huu, kama itaendelea kugawa pointi ambapo hadi sasa imecheza mechi 24.

Matumaini ya Majimaji kubaki kwenye ligi hiyo ni machache, kwani Toto Africans nayo inapigana kuhakikisha haishuki daraja msimu huu, inayoshika nafasi ya 14 kwenye msimamo kutokana na pointi 25.

Pamoja na timu hizo kuwa katika mazingira magumu ya kushuka daraja, Ndanda nayo haiko nafasi nzuri sana ya kujihakikisha kubaki kwenye ligi hiyo.

 

Ndanda inayofundishwa na Meja Mstaafu wa Jeshi, Abdul Mingange, ana kazi ngumu ya kuibakisha timu hiyo inayoshika nafasi ya 12 kutokana na pointi 27.

 

Ndanda haiko katika nafasi bora zaidi, kwani inatakiwa kushinda mechi zake zilizosalia ili kujihakikisha kuwemo katika timu 16 zitakazoendelea kushiriki ligi hiyo msimu ujao.

Meja Mingange anatakiwa kufanya kazi ya ziada ili Ndanda isimfie mikononi mwake na kujikuta akiingia katika rekodi mbaya ya kushusha timu daraja.

Baadhi ya makocha wameingia kwenye rekodi ya kushusha timu Ligi Kuu Bara, kitu ambacho sitarajii kukiona kwa Meja Mingange akiishusha Ndanda msimu huu.

 

Tukutane Jumatatu ijayo

kapssmo@gmail.com 0716985381

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -