Saturday, November 28, 2020

MESEJI SENT, YANGA YAPIGA MTU 6 – 0

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

Yanga imetuma ujumbe na bila shaka umepokelewa vyema na timu zinazoshiriki ubingwa wa kombe la mapinduzi linaloendelea mjini unguja.

MUZIKI wa Yanga ndio huo ambayo umeanza kusikika Visiwani Zanzibar katika michuano yaKombe la Mapinzuri baada ya kuizabua bila huruma Jamuhiri ya Pemba kwa mabao 6-0.

Kocha wa Yanga, George Lwandamina alianza kupanga kikosi kizima kilichojaa nyota wake wote ambacho ndio hasa unaweza kukiita kikosi cha kwanza cha Yanga kinachotarajiwa kwa wakati huu na kwenye michuano ya kimataifa.

Kama ambavyo Gazeti la BINGWA liliandika jana kwamba kocha huyo aliwapa kapu ili washambuliaji wake walijaze mabao ambapo aliwataka kufunga mabao mengi zaidi katika kila mechi na ndiyo iliyotokea.

Kocha huyo alielezwa kuweka mpango wa timu hiyo kupata mabao zaidi ya manne katika kila mechi na kumaliza michuano ya mapinduzi wakiwa na mabao 20 jambo ambalo linaonekana linaweza kutimia kweli.

Katika mchezo huo wa jana bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Simon Msuva ambaye aliunganisha kwa kichwa kona nzuri iliyochongwa na Haruna Niyonzima.

Yanga iliendelea kulishambulia lango la Jamhuri kwa kasi huku ikionekana kumiliki zaidi eneo la kiungo lililokuwa na viungo wake watatu wa kutumainiwa, Niyonzima, aliyecheza kama namba 10, Justin Zulu aliyecheza kiungo mkabaji huku Thaaban Kamusoko (TK) akicheza kiungo wa kati.

Mashambulizi hayo ya Yanga yalizaa matunda tena katika dakika ya 23, kwa bao la Donald Ngoma ambaye aliunganisha krosi safi ya Mwinyi Haji ambaye kabla ya kupiga krosi hiyo aligongeana vyema na Emmanuel Martin

Ngoma alifunga bao hilo kirahisi sana kwani alitaka kuutuliza mpira lakini ukawamzidi na kwa bahati nzuri kwa Yanga na kwake Ngoma mpira huo ulimpita pia kipa wa Jamhuri Omar Said na kuingia wavuni.

Bao la tatu la lilifungwa katika dakika ya 37, likifungwa na Ngoma ambaye alimalizia mpita uliopanguliwa na kipa wa Jamhuri ambaye aliokoa shuti la Msuva. Zulu alifanya kazi nzuri ya kuwachambua viungo wa Jamhuri na kisha kumuwekea Niyonzima ambaye alimpasia Ngoma naye akamtengea Msuva aliyeachia shuti lililopanguliwa na kipa kisha kumkuta Ngoma aliyemalizia.

Mashambulizi ya Yanga hayakukokoma kwani waliendelea kulisakama lango la Jamhuri kwa kasi kubwa na walifanikiwa kupata bao la nne likifungwa na Msuva  dakika ya 40, ambaye alitumia vyema makosa ya beki wa Jamhuri aliyeshindwa kuokoa pasi ndefu ya Kamusoko na kisha Msuva akamvisha kanzu kipa na kuipa Yanga bao la nne.

Kipindi cha pili kilinza kwa Jamhuri kujipanga vilivyo na walionekana kutulia zaidi na kuanza kwa kulishambulia lango la Yanga huku wakifanya mashambulizi makali ambayo hata hivyo hayakuzaa matunda.

Kamusoko aliiandikia Yanga bao la tano dakika ya 59 akiunganisha kwa kichwa krosi safi ya Martin kutoka wingi ya kushoto. Yanga walifanya mabadiliko zaidi kwa kuwatoa Niyomzima na nafasi yake kuchukuliwa na Deus Kaseke,  na baadaye akatoka Ngoma na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi.

Juma Mahadhi aliifungia Yanga bao la sita  kwa shuti kali kufuatia mpita wa kona uliookolewa na beki wa Jamuhiti na kumkuta mfungaji akiwa ndani ya eneo la hatari.

Katika mchezo wa mapema Azam FC, nayo ilianza vema mashindano hayo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimamoto katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Amaan.

Bao pekee la ushindi kwa Azam lilifungwa katika dakika ya 79 kupitia kwa mchezaji, Shabani Iddy, aliyempiga kanzu kipa wa Zimamoto na kasha kuukwamisha mpira kimiani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -