Friday, December 4, 2020

MESSI WA MFUKO WA ‘PLASTIKI’ ALIVYOMGANDA MESSI ‘ORIJINO’

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

Doha, Qatar

Mtoto wa Afghanistan ambaye alipata umaarufu baada ya kuvaa mfuko wa ‘plastiki’ wenye mistari kama jezi ya Argentina na kuandikwa mgongoni jina Messi (Lionel Messi), hakutaka kuondoka kumwachia nyota huyo wa Barcelona baada ya kumsindikiza uwanjani.

Murtaza Ahmadi mwenye umri wa miaka mitano, alikuwa msindikizaji wakati Barca wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Al Ahli mjini Doha juzi Jumanne usiku baada ya kukutana na Messi mapema kabla ya mechi hiyo.

Wakati miamba hiyo ya La Liga ilipokuwa ikipiga picha ya kikosi, Ahmadi alikimbia na kuungana na Messi na kusimama mwisho wa mstari na Messi kumshika mkono na kupiga naye picha.

Nyota huyo wa Argentina aliendelea kuwa naye kwa kuwa Murtaza kutoka uwanjani na kumfanya Luis Suarez kucheka muda wote, kabla ya mwamuzi kumtoa nje mtoto huyo.

Murtaza aliishtua dunia nzima, baada ya picha yake aliyokuwa amevaa mfuko huo wa ‘plastiki’ ukiwa umeandikwa namba 10 mgongoni kuzagaa.

Baada ya kuzagaa kwa picha hiyo, nyota huyo wa Barcelona alimtumia mtoto huyo jezi ya Argentina ikiwa imesainiwa, lakini sasa mambo yamekuwa tofauti baada ya kukutana ‘live’ Messi huyo wa mfuko wa plastiki na Messi ‘origino’.

“Picha ambayo dunia ilitamani kuiona,” iliandikwa kwenye akaunti ya mtandao wa Twitter wa Kamati ya Wandaaji wa Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar. “Kijana mdogo aliyekuwa na ndoto za kukutana na shujaa wake Messi, hatimaye ndoto yake imekuwa kweli.”

Ahmadi alisafirishwa kutoka mashariki mwa Ghazni nchini Afghanistan, Mei mwaka huu na kwenda Pakistan kukimbia machafuko.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -