Monday, October 26, 2020

MEXIME AWAITA MASHABIKI MUSOMA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA GLORY MLAY


 

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime,  amewaalika mashabiki wa kikosi hicho, kufika kwa wingi kesho Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Musoma  mkoani Mara, kushuhudia mechi yao na Biashara United.

Huo ni mchezo wa tatu kwa timu hiyo, ikijivunia nafasi ya nane iliyopo kwa kujikusanyia pointi nne sawa na Singida United, baada ya kucheza michezo miwili na kushinda mmoja huku wakitoka sare mmoja.

Akizungumza na BINGWA jana, Mexime, alisema anataka mashabiki wake washuhudie jinsi atakavyochukua pointi tatu ugenini kutokana na kuimarika kwa kikosi chake.

“Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wa kesho, vijana wangu wote wapo sawa na matarajio yetu ni kupata ushindi ambao utatuongezea ari ya kufanya vizuri mechi zinazokuja,” alisema Mexime.

Alisema anaamini mchezo utakuwa mgumu lakini wamejipanga kwa sababu amesharekebisha makosa katika michezo ya nyuma.

“Mara ya mwisho tulipoteza mchezo mmoja, lakini kikosi changu cha msimu huu kipo tofauti kidogo na msimu uliopita ambapo wachezaji wengi wameonyesha kujituma na kuhakikisha wanailetea timu hiyo mafanikio,” alisema Mexime.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -