Monday, August 10, 2020

Mfaransa kocha mpya Yanga

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA ZAINAB IDDY

IWAPO mambo yatakwenda vizuri, Mfaransa Diego Garzitto ndiye atakayebeba mikoba ya kocha wa Yanga aliyetimuliwa, Luc Eymael, imefahamika.

Garzitto, beki wa zamani wa klabu za CS Louhans-Cuiseaux na AC Ajaccio, Mfaransa aliyezaliwa Italia, ni moja ya makocha wenye uzoefu wa kutosha, akiwa amepata mafanikio lukuki katika timu alizowahi kufundisha.

Kocha huyo aliyeanza kufundisha soka mwaka 1984 akiwa na klabu ya CS Louhans-Cuiseaux ya Ufaransa, amevinoa vikosi lukuki vya nchini kwao, vikiwamo vya klabu na mataifa mbalimbali Afrika.

Garzitto alianza kutia mguu katika ardhi ya Afrika pale alipopata dili la kuifundisha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Ethiopia, mwaka 2001.

Baada ya hapo, aliinoa timu ya Taifa ya Togo (2002) kabla ya kunyakuliwa na TP Mazembe (2003–2004) na baadaye kubebwa na        klabu ya CS Louhans-Cuiseaux ya Ufaransa.

Mwaka 2006 hadi 2007, aliifundisha timu ya Taifa ya Ethiopia kabla ya kurejea TP Mazembe (2009-2010) na baadaye kuzinoa klabu kadhaa kubwa Afrika kama Wydad Casablanca (2010-2010), Al-Hilal Omdurman (2012-2013       ), CS Constantine (2013), Al-Merrikh (2014-2016) na Al-Ittihad (2017).

Mafanikio yake

Garzitto ni kocha wa mataji akiwa amebeba kombe la michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na TP Mazembe mwaka 2009.

Akiwa na kikosi cha Al-Merrikh ya Sudanm, mwaka 2015 alitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo na Kombe la Ligi kabla ya kuiwezesha timu hiyo kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Katika hatua hiyo ya nusu fainali, Al-Merrikh ilitolewa na TP Mazembe waliokuwa mabingwa kabla ya kutua katika klabu ya FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo anayoinoa hadi sasa.

Kutokana na wasifu wake huo, hasa uzoefu wake katika soka la Afrika, ukiwamo umahiri wake wa kutwaa mataji makubwa kama la Ligi ya Mabingwa Afrika, ni wazi Garzitto atakuwa mtu sahihi wa kubeba mikoba ya Eymael.

Habari ambazo BINGWA limezinasa juzi usiku kutoka kwa rafiki wa kocha huyo, zinasema kuwa tayari Garzito ameanza mazungumzo na wawakilishi wa Yanga ili kubeba mikoba ya Eymael.

“Yanga wameanza mazungumzo na kocha Garzito ambaye hana mahusiano mazuri na uongozi wa klabu yake ya FC Saint Eloi Lupopo. Ni kocha mzuri ambaye anaonekana kuwa na kiu ya mafanikio.

“Japo Lupopo bado wanamuhitaji, lakini anaonekana hafurahishwi na jinsi klabu hiyo inavyoendeshwa, zaidi ikiwa ni suala zima la usajili kwani haletewi wachezaji anaowataka,” alisema rafiki huyo wa Garzito.

BINGWA jana lilimtafuta mwanahabari wa michezo nchini DR Congo, Jean-claude Sefu ili kufahamu iwapo ana taarifa juu ya mpango huo wa Garzito kutua Yanga na kwamba alikiri hilo.

“Ni kweli nimesikia hilo, tayari kocha Garzito yupo katika mazungumzo na Yanga ya huko Tanzania na viongozi wa FC Lupopo wamepata taarifa hizo hivyo wanaendelea kupambana ili wabaki naye, japo sidhani kama watafanikiwa,” alisema.

Kwa upande wa Yanga, wadhamini wa klabu hiyo, Kmapunui ya GSM kupitia Mkurugenzi wa Uwekezaji, Mhandisi Hersi Said, ameliambia BINGWA kuwa ni mapema mno kuzungumzia suala la kocha kwani wanahitaji kuwa makini mno katika hilo.

Alisema kuwa azma yao ni kukijenga upya kikosi cha Yanga, kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji ili msimu ujao waweze kuwa moto wa kuotea mbali Ligi Kuu Tanzania Bara.

Toka ameachana na Al Ittihad Tripoli ya Libya mwaka 2018, Garzito hakuwa na timu ndipo alipoamua kurejea ‘mzigoni’ mwaka huu kukinoa kikosi cha FC Saint Eloi Lupopo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -