Saturday, October 31, 2020

MFUMO HUU WA CHELSEA UTAIMALIZA ARSENAL EMIRATES

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

London, England

Chelsea wanakutana na Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, utakaopigwa kesho saa 1:30 usiku, katika Uwanja wa Emirates.

Baada ya Chelsea kuichapa Leicester City mabao 4-2 kwenye mchezo wa English Football League Cup (Kombe la Ligi), kocha wa Blues, Antonio Conte, kesho atakuwa na kazi ngumu kuchagua kikosi kitakachoanza dhidi ya Gunners.

Conte atahitaji kutumia mbinu zake awezavyo ili kuweza kupata ushindi wake wa kwanza kwenye mechi kubwa, baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Liverpool wiki iliyopita.

Chelsea walionekana kuukosa uwepo wa kiungo wao, Cesc Fabregas, kwenye mechi dhidi ya Liverpool, lakini mabao yake mawili dhidi ya Leicester lazima yatamfanya awemo katika wachezaji wanaogombania namba kwenye kikosi cha kwanza.

Lakini kuna maamuzi mengine kadhaa kwa Conte kufikiria kuyafanya siku chache zijazo, wakati watakapokutana na Arsenal kesho na huenda wakaichapa Arsenal kwenye uwanja wao wa Emirates wakitumia mfumo wa 4-3-2-1.

Itakuwa sahihi kabisa kusema kwamba kati ya wachezaji waliofanya vibaya katika mchezo dhidi ya Liverpool ni Branislav Ivanovic na Gary Cahill.

Cesar Azpilicueta alicheza vizuri dhidi ya Leicester baada ya kuhamishwa kutoka kushoto hadi kulia, upande wa beki wa kushoto alicheza Marcos Alonso, ambaye naye alionyesha kiwango.

Mkongwe John Terry anaweza kurejea kwenye kikosi cha Chelsea dhidi ya Arsenal, ila macho yote yatakuwa kwa David Luiz, ambaye anatarajiwa kucheza mechi yake ya pili katika kikosi hicho baada ya mechi yake ya kwanza dhidi ya Liverpool, alionekana kuwa tegemeo zaidi kwa Cahill.

Iwapo Terry atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo, Conte anapaswa kumpanga sambamba na Luiz.

Kutokana na Chelsea kushindwa kuwa wabunifu kwenye safu ya kiungo katika mechi dhidi ya Liverpool, Fabregas anapaswa kurudishwa kuivaa klabu yake hiyo ya zamani. Baada ya mabao yake mawili katika Uwanja wa King Power juzi Jumanne, anaonekana kuwa muhimu sana kwenye mchezo huo.

Nyota huyo wa Hispania atataka kuonyesha cheche zake Chelsea baada ya kuwa na hofu juu ya hatima yake kwenye kikosi hicho cha Blues.

Nemanja Matic alikuwa dhaifu kwenye kukaba na kutengeneza mashambulizi, bila shaka mchezaji ambaye anaweza kushirikiana na Fabregas ni N’Golo Kante, ambaye alipumzishwa kwenye mechi ya EFL Cup (English Football League).

Huenda Chelsea wakaamua kumtumia Pedro kama kiungo mshambuliaji (namba 10) baada ya kiwango chake alichoonyesha dhidi ya Leicester, lakini inaonekana wazi kwamba Conte ataendelea kutumia wachezaji wake watatu; Eden Hazard, Oscar na Willian.

Nafasi ya ushambuliaji kwa Diego Costa hilo halina shaka, kutokana mshambuliaji huyo kuongoza kwa mabao msimu huu, baada kufumania nyavu mara tano Ligi Kuu England na anaonekana kuwa vizuri sana msimu huu tangu ametua kwenye klabu hiyo ya Stamford Bridge.

Costa pia ndiye aliyefunga bao la ushindi kwenye Uwanja wa Emirates msimu uliopita, ambapo amekuwa kama Didier Drogba kutokana na kusumbua Gunners kila wanapokutana tangu ametua Chelsea.

Chelsea walishindwa kufanya vizuri dhidi ya Liverpool wakiwa nyumbani Stamford Bridge wiki iliyopita, ila wakitumia mfumo huo wa 4-3-2-1 bila shaka Conte anaweza kuibuka na ushindi Emirates.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -