Wednesday, October 28, 2020

MGAWANYIKO Mpango wa Waarabu kuimiliki Manchester Utd waibua mapya

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MANCHESTER, England

MASHABIKI wa Manchester United wameingia katika mgawanyiko juu ya mpango wa Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammad bin Salman, kutaka kuimiliki klabu yao hiyo.

Bin Salman alionesha nia hiyo ya kutaka kuinunua Man United kutoka kwenye familia ya Glazer, ambayo wanaimiliki klabu hiyo tangu mwaka 2005, ili kumpa upinzani mkali mmiliki wa Man City, Mansour bin Zayed Al Nahyan.

Kutokana na Saudi Arabia kukabiliwa na skendo ya mauaji ya mwandishi wa habari mkosoaji yaliyotokea hivi karibuni, mpango huo huenda usiwe hatua nzuri kwa klabu ya Man Utd.

Hata hivyo, wawekezaji wengi wameonesha kuvutiwa na taarifa za mpango huo, kiasi cha kuipandisha thamani ya Manchester United (kampuni) katika soko la hisa kwa zaidi ya asilimia tano.

Kwa mashabiki wa United, kumeibuka mgawanyiko wa maoni juu ya mpango huo wa Bin Salman kutaka kuinunua klabu yao hiyo.

Baadhi yao wanaamini kama Bin Salman ataruhusiwa kuinunua klabu hiyo kwa kitita kinachokadiriwa kuwa pauni bilioni tatu hadi nne, itakuwa ni hatua chanya kwao na itasaidia klabu hiyo kujikwamua kutoka kwenye madeni.

“Huenda hii ikawa ndiyo nafasi yetu kuwa na wamiliki wanaotaka tuwe na timu bora duniani na si sehemu ya watu kujichotea faida,” aliandika mmoja wa mashabiki hao katika mtandao wa Twitter.

“Mbona watu wanalalamika sana,” mwingine aliongeza. “Hili ni jambo jema kwa klabu yetu. Kama wanataka kulipa pauni bilioni tatu hadi nne ili kuinunua klabu, basi wataweza kulipa deni la pauni milioni 700!

Lakini, baadhi ya mashabiki wengine wa Man Utd wamefika mbali hata kugusia rekodi mbovu ya haki za binadamu waliyonayo viongozi wa Saudi Arabia.

“Kama ni suala la uwekezaji sina tatizo. Ila kwa klabu yoyote yenye nidhamu, inayoheshimika duniani, huu mpango ni tatizo kubwa,” shabiki mwingine alipaza sauti yake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -