Saturday, November 28, 2020

MGOMO MKUBWA WANUKIA YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU


MGOMO wa siku mbili uliofanywa na wachezaji wa Yanga wakidai mishahara yao, ni cha mtoto na ilikuwa ni ishara tu ya mgomo mkubwa zaidi, BINGWA limedokezwa.

Mgomo huo au mgogoro huo ambao unanukia baina ya wachezaji na uongozi wa klabu hiyo, unatokana na madai ya maboresho ya mishahara kwa nyota kadhaa wa timu hiyo ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa uwanjani lakini wanalipwa kiduchu.

Sakata la mgomo wa wachezaji wa Yanga, lilianza kunukia tangu mara baada ya mechi ya JKT Ruvu, ambapo baadhi ya vigogo wa timu hiyo walianza kuhoji kwanini baadhi ya wachezaji wanalipwa fedha nyingi halafu hawana msaada wowote kwenye timu.

“Tumekuwa tukilalamikiwa na baadhi ya watu juu ya mishahara ya wachezaji kadhaa akiwemo Obrey Chirwa, wengi wanasema kwanini Chirwa analipwa kuliko Niyonzima, kwa mfano angalia anachokifanya Niyonzima uwanjani leo hii, halafu angalia Chirwa ameingia dakika ya 92 na hata mpira hakugusa, sasa nani anapaswa kulipwa fedha nyingi, hapa nje mashabiki walikuwa wamenishikilia wananihoji,” anasema mmoja wa vigogo wa Yanga ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini.

Kigogo huyo alisema licha ya kwamba suala la mishahara ni la kimkataba, lakini mashabiki wanahoji kwamba mkataba huo unaweza kupitiwa upya kwa kuwa mchezaji husika hatoi matunda yanayohitajika kulingana na mkataba wake.

Kutokana na maelezo ya kigogo huyo, BINGWA lilikwenda mbali zaidi kuchunguza suala hilo na kubaini kwamba kuna mgomo unaonukia wa baadhi ya wachezaji wa kigeni na wazawa ambao wanatajwa kufanya kazi kubwa lakini wanalipwa kidogo ikilinganishwa na Chirwa ambaye muda mwingi anasugua benchi.

BINGWA lina taarifa kuwa baadhi ya wachezaji wa kigeni wameshaanza kulalamika chini kwa chini wakihoji iweje wanavuja jasho lakini mwingine anayekaa benchi anapokea mshahara mkubwa kuliko wao.

“Hili jambo ni la siri, lakini ukweli ni kwamba baadhi yao wameanza kulalamika na sauti zao sasa zinapaishwa zaidi na mashabiki na viongozi kadhaa.

“Hali hiyo imesababisha wale wanaomaliza mikataba kutaka kuhakikishiwa kama wataongezewa mishahara yao na kumzidi Chirwa vinginevyo wanaweza wakafikia uamuzi mgumu,” kilisema chanzo cha ndani kutoka Yanga.

Kauli hiyo inaakisi kile kilichotokea katika mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo baada ya Chirwa kuanza kupasha misuli dakika za lala salama ili aingie, baadhi ya mashabiki walisema hana msaada wowote na badala yake anakula hela za bure.

“Yaani hata hana msaada wowote ndiyo maana hata kocha ambaye ni ndugu yake, anaamua kumwingiza dakika hizi za nyongeza, anapokea mshahara mkubwa wa bure tu,” alisema shabiki mmoja aliyekuwa jukwaa la watu mashuhuri ambalo siku hiyo walikuwepo pia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.

Mwingine alisema: “Mimi nadhani Haruna Niyonzima ndiye ambaye angestahili kupewa mshahara mkubwa akifuatiwa na Donald Ngoma na Thaban Kamusoko, lakini cha ajabu huyu kilaza (Chirwa) ndiye anayelipwa fedha nyingi.”

Uchunguzi uliofanywa na BINGWA ulibaini kuwa, Chirwa anapokea kiasi cha Sh milioni 10 za Kitanzania kila mwezi, kiasi ambacho ni kikubwa kuliko mchezaji mwingine yeyote ndani ya kikosi hicho cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wakati Chirwa akipokea kiasi hicho, taarifa za ndani zinadai kuwa Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Thaban Kamusoko pamoja na Vincent Bosou, kila mmoja analipwa fedha za Kitanzania Sh milioni 7.6.

Mshahara huo wanaochukua Niyonzima na wenzake wa milioni 7.6 ni tofauti ya milioni 2.4 anazochukua Chirwa hali ambayo hata mashabiki wenyewe wa Yanga wameshaanza kulalamika.

Katika hatua nyingine, jana wachezaji wa Yanga walirudi uwanjani kuendelea na mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -