Tuesday, October 27, 2020

MGOMO WAPANGUA KIKOSI YANGA

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

HUSSEIN OMAR NA MARY PETER, TSJ

MGOMO wa siku mbili walioufanya wachezaji wa timu ya Yanga, huenda ukasababisha mambo makubwa zaidi ndani ya kikosi cha timu hiyo ikiwemo mabadiliko katika kikosi cha kwanza.

Ingawa haijaelezwa waziwazi lakini hali inaonekana kuwa ni hivyo baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina, kuamua kufanya mabadiliko ya ghafla kuelekea katika mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya African Lyon leo kwenye Uwanja wa Uhuru.

Yanga wanatarajiwa kuingia uwanjani jioni hii, huku mashabiki wakiwa na wasiwasi juu ya kupata ushindani hasa kutokana na kadhia ya mgomo na pengine hali hii ndiyo inamfanya kocha huyo kuchekecha kichwa haraka haraka kupanga kikosi ambacho hakitamwangusha.

Katika kikosi kilichopita, Lwandamina aliwaanzisha, Deogratias Munishi, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondan, Vincenti Bussou, Thaban Kamusoko, Deus Kaseke, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Simon Msuva.

Lakini kutokana na mgomo pamoja na mazoezi ya mwisho ya kwenye Uwanja wa Uhuru, Lwandamina alionekana kupangua kikosi huku akimwandaa Emmanuel Martin kucheza pamoja na Niyonzima na Msuva.

Wawili hao, Niyonzima na Msuva kwa sasa wanaonekana kuwa moto wa kuotea mbali katika kikosi cha Yanga kutokana na kiwango ambacho wameanza kukionyesha katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo, lakini pia katika sakata la mgomo Niyonzima na Msuva walionekana kama hawakuunga mkono moja kwa moja.

Katika mazoezi hayo, Lwandamina alitumia muda mwingi kumpika mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Yanga katika dirisha dogo kutoka JKU ya Zanzibar.

Kikubwa kilichoonekana katika mazoezi hayo ni Lwandamina kumpika zaidi fundi huyo wa kufunga mabao baada ya kuelezwa kwamba Ngoma anakabiliwa na majeruhi.

Hata hivyo, huenda pia kukawa na mabadiliko katika nafasi nyingine kulingana na ushauri aliopewa kocha huyo kwani suala la mgomo linaweza likatokea uwanjani ingawa hali imeshakuwa shwari kabisa.

Wachezaji walioonekana kuwa vinara katika mgomo huo wa siku mbili huenda wakaanzia benchi au kuondolewa kwenye kikosi kabisa katika mchezo wa leo.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, hakutaka kuzungumzia suala la mgomo, ingawa alikiri kuharibu programu ya mazoezi ya timu hiyo lakini akasema kwamba watapanga kikosi imara kitakachowapa ushindi.

“Tumejipanga kucheza soka zuri, tunataka tupate mabao mengi yatakayoambatana na burudani safi,” alisema Mwambusi.

Wakati huo huo, mshambuliaji wa timu hiyo, Amissi Tambwe, amesema atahakikisha anafunga bao na kulitoa kama zawadi kwa mwanawe wa kiume, Ayman Tambwe, aliyezaliwa juzi.

Tambwe alisema amefarijika kupata mtoto wa kiume katika ardhi ya Tanzania, baada ya kuishi kwa takribani miaka mitatu.

“Nashukuru Mungu nimepata mtoto wa kiume, hii ni hatua moja mbele katika maendeleo ya maisha yangu, naomba Mungu amjalie afya njema amkuze amwepushe na mabalaa,” alisema Tambwe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -