Tuesday, November 24, 2020

Mguu ndani mguu nje; Huenda timu hizi zikaikosa Urusi 2018

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

NI miezi 12 imebaki kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018, zitakazofanyika Urusi.

Hiyo itakuwa ni mara ya 21 kufanyika kwa michuano tangu ilipoanzishwa mwaka 1930.

Kwa mashabiki wa kandanda, kipute cha fainali za mwaka 2018 kitaanza Juni 14 na kumalizika Julai 15.

Urusi ilipata bahati ya kuandaa michuano hiyo Desemba 2, mwaka 2010 na hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika Mashariki mwa Ulaya tangu ilipotokea 2006.

Jumla ya mataifa 31 yataungana na wenyeji Urusi, nchini humo kuwania taji la michuano hiyo mikubwa duniani.

Hata hivyo, hivi karibuni kulikuwa na michezo kadhaa ya kuwania kufuzu fainali hizo.

Baada ya mechi hizo, kuna wasiwasi mkubwa kuwa baadhi ya timu kubwa zinaweza kushindwa kukata tiketi ya kwenda Urusi mwaka 2018.

Argentina

Argentina walikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa mahasimu wao, Brazil na hayo hayakuwa matokeo mazuri kwa upande wao.

Argentina wamebaki nafasi ya tano, licha ya kushindi mabao 3-0 katika mchezo uliofuata dhidi ya Colombia.

Bado kikosi hicho kina kazi nzito kuhakikisha kinashinda mechi sita zilizobaki, kwani Brazil na Uruguay wanapewa nafasi kubwa ya kwenda kwenye fainali hizo.

Ghana

Black Stars wamefuzu katika fainali tatu zilizopita na mwaka 2010 waliishia hatua ya robo fainali.

Kama ilivyo kwa Argentina, nafasi yao ya kutua Urusi ni ngumu.

Baada ya kutofungana na Uganda na kisha kufungwa na Misri, wanashika nafasi ya tatu kwenye kundi ambalo ni timu moja tu ndiyo itakayokata tiketi ya kwenda Urusi.

Misri wana uhakika wa asilimia 100 kucheza fainali hizo na kama watafanikiwa itakuwa ni mara yao ya kwanza tangu mwaka 1990.

Lakini pia, hiyo itakuwa ni mara yao ya tatu kucheza michuano hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1930.

Uholanzi

Baada ya kuzikosa fainali za Euro 2016, bado hakuna uhakika wa Uholanzi kushiriki mashindano ya kombe la dunia.

Huenda ikakwama kwenye kundi lao lenye Ufaransa na Sweden.

Tayari Uholanzi ambao walizikosa fainali za mwaka 2002, wameshapoteza mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Ufaransa.

Ufaransa wanaoongoza kundi wamewaacha Uholanzi kwa pointi tatu.

Uholanzi wanaipigania nafasi ya pili, wakilingana pointi na Sweden.

Ureno

Mabingwa hao wa Euro 2016 wako kwenye wakati mgumu kuhakikisha wanakwenda Urusi.

Ureno wamepoteza mchezo mmoja katika mechi za kufuzu, lakini Uswis wameshinda yote.

Ni wazi Uswis watahitaji sare tu katika mchezo wa Agosti 31 dhidi ya Ureno na hapo watakuwa wamefuzu.

Ambacho kinaweza kuwamaliza Ureno ni tofauti ya mabao, huku Hungary wakiwa nyuma yao kwa tofauti ya pointi mbili tu.

Marekani

Marekani ya kocha Jurgen Klinsmann haijaambulia pointi katika michezo miwili.

Kipigo cha mabao 4-0 walichokipata juzi kutoka kwa Costa Rica kimezidi kuharibu hali ya hewa.

Kuna taarifa kuwa, huenda matokeo hayo yakamfukuzisha kazi Mjerumani Klinsmann.

Katika kundi lao, ni timu tatu kati ya sita ndizo zitakazofuzu moja kwa moja kwenda Urusi.

Moja kati ya mwenendo mbovu wa Marekani ni kushindwa kutumia uwanja wa nyumbani na kukubali kipigo kutoka kwa Mexico.

Lakini, hali itakuwa mbaya zaidi ikiwa Marekani itashindwa kuzoa pointi dhidi ya vibonde Honduras, Panama na Trinidad & Tobago.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -