Tuesday, November 24, 2020

Michael Jackson anavyopiga pesa akiwa kaburini

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LOS ANGELES, Marekani

WENGI wanaamini kuwa mwisho wa kila jambo kwa binadamu ni pale anapoiaga dunia. Si kweli.

Kuna baadhi ya mambo yako yataendelea kubaki ulimwenguni hata baada ya wewe kuondoka.

Mfano; mbali na ngoma kali alizotuachia mwanamuziki Michael Jackson, lakini pia kuna jambo lake jingine limeendelea kuishi na sisi. Hakuondoka na utajiri wake.

Wiki iliyopita jarida maarufu la Forbes ‘lilimfufua’ staa huyo aliyeiaga dunia mwaka 2009.

Taarifa za utajiri wake iliyotolewa na jarida hilo imeacha gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Forbes lilimtaja mkali huyo kuwa ndiye mwenye kipato kikubwa kuliko mastaa wote waliofariki dunia.

Kwa maana nyingine, mkali huyo wa Pop amendelea kuingiza fedha nyingi hata baada ya kuiaga dunia na kuwafunika wenzake waliotangulia mbele ya haki.

Lakini pia mbali na wenzake hao kipato cha Michael kwa mwaka huu kimewafunika hata mastaa wanaoendelea kufanya kazi.

Yaani tangu kuanza kwa mwaka huu hakuna staa aliyeingiza fedha nyingi kama Michael.

Si Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Jose Mourinho, Neymar, Jay Z, P. Diddy, Kanye West, Rihanna, Lil Wayne, Drake, wala unayemfikiria na ambaye hajatajwa hapa.

Ikiwa ni miezi 10 pekee imepita tangu kuanza kwa mwaka huu, utafiti wa Forbes umebaini kuwa tayari Michael ameshaingiza kiasi cha dola za Marekani milioni 825.

Kwa mujibu wa mmoja wa wanasheria wake alipokuwa akihojiwa na mtandao wa IBTimes UK, eneo analomiliki Michael lina thamani ya dola bilioni 1.

Mwezi uliopita mwanasheria wake huyo, Brian Panish, alisema: “Sijatazama makabrasha ya sasa lakini kiasi hicho kinaweza kufika. Kuna makabrasha yaliyopo mahakamani, nadhani eneo lake linaweza kuzidi kiasi hicho.”

Pia Panish aliongeza kuwa ardhi hiyo ya Jackson ambayo ilikuwa ikidaiwa kodi mwaka 2009 imeshalipiwa.

“Kulikuwa na kiasi fulani cha deni lakini kimeshalipwa.”

Imeelezwa kwa moja kati ya vitu vilivyomwongezea kipato ni mkataba na Kampuni ya Sony ambapo familia yake imechukua dola milioni 750.

Wakati wa uhai wake, Michael alijijengea umaarufu mkubwa kutokana na tungo na aina yake ya utumbuizaji.

Kwa kipindi hicho,  jarida la Forbes liliweka wazi kuwa shughuli hizo za muziki zilimuingizia zaidi ya dola milioni 100.

Lakini pia, mbali na ngoma zake zilizokuwa zikifanya vizuri sokoni, alikuwa akilipwa fedha nyingi kila aliposhirikishwa kwenye kazi za wasanii wenzake.

Miongoni mwa ngoma kali ambazo mpaka leo zimebaki kwenye kumbukumbu za wapenzi hasa ule wa Pop ni, ‘Shake Rattle and Roll’, ‘Runaround Sue’, ‘Great Balls of Fire’, na ‘When a Man Loves a Woman’.

Moja kati ya rekodi zilizowahi kuwekwa na Michael katika kazi yake ya muziki ni pale alipouza nakala milioni 98, huku idadi hiyo ikiwa ni ile iliyosambazwa Marekani pekee mbali na sehemu nyingine duniani.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2009 mkali huyo aliuza nakala milioni 24 nje ya soko la muziki la nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Forbes kwa kipindi hicho, mauzo hayo yalimfanya Michael kuingiza dola milioni 383 kwenye akaunti yake.

Kwa upande mwingine mbali na muziki, Michael alichota mpunga wa kutosha kutokana na kazi ya uigizaji.

Moja kati ya filamu iliyompa fedha nyingi ni ile iliyokwenda kwa jina la ‘This Is It’.

Vyanzo mbalimbali vya habari vimedai kuwa ni muvi hiyo ndiyo iliyomwingizia zaidi ya dola milioni 500.

Inasemekana kuwa Michael aliuandaa ‘mzigo’ huo kwa kushirikiana na wanasheria wake.

Filamu hiyo ni muunganiko wa video zake binafsi akiwa nyumbani pamoja na kipindi cha mwisho kabla ya kuiaga dunia.

Ukiachana na filamu, pia Michael alijikusanyia dola milioni 250 baada ya kukubali kuuza hatimiliki ya kazi zake za muziki kwa Sony.

Taarifa nyingine zimeongeza kuwa hilo ndilo lililokuwa dili kubwa kuliko yote katika historia ya muziki.

Kwa maana nyingine basi, hakuna msanii mwingine wa muziki ambaye amewahi kupata mkataba mnono kama huo.

Dili jingine kali ambalo msanii huyo amewahi kufaidika nalo na kuingiza fedha nyingi ni lile la Pepsi.

Michael aliingia mkataba na kampuni hiyo ya vinywaji ambapo alikubali picha zake zitumike katika matangazo ili kuwavutia wateja.

Huyo ndiye Michael Jackson. Amekula maisha akiwa hai na sasa anaingiza fedha akiwa kaburini.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -