Saturday, November 28, 2020

MICHAEL PHELPS: MKALI WA KUOGELEA MWENYE REKODI ZA KUSHANGAZA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ALEX VULIVER, TSJ

MCHEZO wa kuogelea ni miongoni mwa michezo maarufu kwa nchi za Magharibi na duniani kwa ujumla, huku ukiwa ni moja ya matukio yanayotambulika na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC).

Katika mchezo wa kuogelea, wapo watu mbalimbali ambao wamefanya makubwa na kuishangaza dunia kutokana na umahiri waliokuwa nao.

Michael Phelps aliyezaliwa Juni 30, mwaka 1985 katika Kitongoji cha Baltimore mjini Maryland, Marekani, ni miongoni mwa wakali wa mchezo huo anayeheshimika mno kila pembe ya dunia.

Mkali huyo anashikilia rekodi ya muda wote kwenye michuano ya Olimpiki akiwa kama mwogeleaji aliyetwaa medali 23 za dhahabu akiwa kinara katika michuano hiyo kwa awamu tofauti.

Baba wa mkali huyo ambaye ni Michael Phelps, ni askari mstaafu wa Jeshi la Nchi Kavu lililojulikana kama Mary State Trooper na alishawahi kuwa mwanamichezo ambapo aliwahi kucheza soka akiwa sekondari na mwaka 1970 aliichezea timu ya Washington Redskin.

Phelps alianza kujikita katika uogeleaji akiwa na umri wa miaka saba ambapo dada zake, Hilary na Whitney, ndio waliomhamasisha kuupenda mchezo huo.

Mwaka 2000, Phelps akiwa na umri wa miaka 15, alishiriki michuano mikubwa ya mchezo wa kuogelea katika mashindano ya olimpiki akafanikiwa kutinga hatua ya fainali, akitumia mtindo wa Butterfly na kukamata nafasi ya tano na kuwa mwogeleaji mwenye umri mdogo kuunda timu ya Taifa ya kuogelea ya Marekani, hata hivyo hakufanikiwa kutwaa medali kwa kipindi hicho.

Machi 30, mwaka 2001, Phelps alishiriki michuano mikubwa ya dunia ya kuogelea kwa vijana wadogo iliyojulikana kama World Acquatics Championship iliyofanyika nchini Japan, ambapo mkali huyo alifanikiwa kuvunja rekodi akiwa kijana mwenye umri wa miaka 15 na miezi 9 kuwa bingwa kwa kushinda mita 200 akitumia mtindo wa butterfly.

Hapo awali rekodi hii ilikuwa ikishikiliwa na Ian Thorpe ambaye alifanikiwa kushinda kwa kuogelea mita 400 akitumia mitindo yote (freestyle) akiwa kijana mwenye umri wa miaka 16 na miezi mitatu.

Mwaka 2003, Phelps alishiriki michuano ya dunia ya kuogelea iliyofanyika nchini Australia ambapo mkali huyo alifanikiwa kukamata nafasi ya kwanza, ambapo raundi ya kwanza aliogelea mita 200 kwa mtindo wa kawaida, raundi ya pili mita 200 kwa mtindo wa kinyumenyume (backstroke) na ya tatu mita 100 kwa mtindo wa butterfly na kuweka rekodi ya kuwa Mmarekani wa kwanza kushinda michuano hiyo kwa mitindo tofauti.

Katika mwaka huo wa 2003, Phelps alifanikiwa kutwaa medali nne za dhahabu na mbili za shaba katika michuano iliyojulikana kama Word Acquatic Championship.

Mwaka 2006 Phelps alifanikiwa kuweka rekodi nyingine kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye michuano ya Pan Passific Champions ships ambayo inashirikisha nchi zilizopo ukanda wa passific. Mkali huyo alitumia dakika 1:54 akimshinda Ryan Lotche aliyetumia dakika 1:56 akimwacha kwa sekunde mbili.

Mwaka 2008 Phelps alishangaza dunia baada ya kuweka rekodi ya kutwaa medali nane za dhahabu katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika Beijing nchini China na kuwa muogeleaji wa kwanza kutoka Marekani akishinda mita mia kwa mizunguko minne akitumia mtindo huru (free style).

Phelps aliendeleza makali yake kwa mara nyingine mwaka 2012 katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika London akitwaa medali nne za dhahabu na mbili za shaba. Mkali huyo alistaafu kuogelea kwa mara ya kwanza baada ya michuano hiyo.

Mwaka 2014 Phelps alitangaza kurejea tena na kuendelea kushiriki mchezo wa kuogelea, akishiriki mashindano mbalimbali kama Word Aquatics Championship yaliyofanyika nchini Marekani kwa lengo la kuandaa timu ya taifa ambayo ingeshiriki katika michuano ya Olimpiki ya mwaka 2016 Rio de Janeiro, Brazil.

Mwaka 2016 katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil, Phelps alidhihirisha umahiri wake katika mchezo wa kuogelea, akifanikiwa kutwaa medali tano za dhahabu na moja ya shaba.

Mkali huyo amefanikiwa kuweka rekodi ya muda katika michuano ya Olimpiki, akiwa ni miongoni mwa wanamichezo waliotwaa medali nyingi katika mashindano hayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -