Friday, October 30, 2020

MICHAEL SCHUMACHER BADO YUKO HAI?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MUNICH, Ujerumani

KAULI ya meneja wa dereva wa zamani wa mbio za magari ya Formula 1, Michael Schumacher, imeibua hofu kuhusiana na uhai wa mkongwe huyo.

Meneja huyo, Willi Weber, ameikosoa familia ya Schumacher akidai kwamba inaficha ukweli kuhusiana na hali yake.

Dereva huyo wa Ujerumani, alipata majeraha makubwa ya kichwa alipokuwa akicheza mchezo wa kukimbia mwaka 2013 na amekuwa akitunzwa nyumbani tangu mwaka 2014.

Alikuwa amewekwa chumba maalumu, lakini hajawahi kusikika wala kuonekana mpaka sasa.

Mwezi uliopita, picha ya kwanza ya bingwa huyo wa mbio za magari mara saba ilikuwa ikiuzwa Ulaya kwa pauni milioni 1.

Hivyo Willi anakosoa kukosekana kwa taarifa, jambo ambalo limewafanya wengine waanze kuhoji kama Schumacher yuko hai au amekwishafariki na familia hiyo imeamua kuficha.

“Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikisema kwamba familia ya Schumacher haisemi ukweli,” Willi aliliambia jarida la Bunte.

“Lakini nimeamua kuuchuna kwa kuwa ni muda mrefu sasa ushauri wangu hausikilizwi.

Lakini kauli ya Willi ambayo ilitia hofu watu juu ya uhai wa Schumacher, ni ile aliyosema: “Ninapokuwa nyumbani peke yangu na simu inapoita mara zote nahisi atakuwa ni Michael anataka kuniambia ‘Willi, unaendeleaje?”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -