Friday, December 4, 2020

Michezo imerudi, wachezaji sasa kuvuna walichopanda

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

RAIS Dk. John Magufuli ameruhusu shughuli za michezo, ikiwamo Ligi Kuu Tanzania Bara kurejea kuanzia Juni Mosi, mwaka huu, ikiwa ni baada ya kusimamishwa tangu Machi 17, mwaka huu.

Serikali ilisimamisha shughuli za mikusanyiko, ikiwamo michezo kutokana na hofu ya kuenea kwa maambukizi ya virus vya corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 unaoitesa Dunia kwa sasal.

Ugonjwa huo ulioanzia China, umepiga hodi katika mataifa mbalimbali, yakiwamo yaliyoendelea kiuchumi na kusababisha vifo vya wengi, huku kukiwa na kesi lukuki za walioambukizwa.

Ni kutokana na hali hiyo, serikali za mataifa mbalimbali zilipiga marufuku shughuli zote za mikusanyiko, ikiwamo michezo ili kuepusha hatari ya maambukizi ya virus hiyo, kwa kitaalam vikifahamika kama Covid-19.

Nchini Tanzania, nasi hatukuachwa na virus hivyo, vikiwa vimesababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wakiwa wameathirika na ugongwa huo.

Pamoja na hali hiyo, Rais Magufuli juzi alitangaza kuruhusu michezo iendelee kuanzia Juni Mosi baada ya kuanza kupungua kwa maambukizi ya virus cya corona, lakini akisisitiza kuchukuliwa kwa tahadhari ya kujikinga na janga hilo kama inavyoshauriwa na wataalam wa afya.

Kwa kipindi ambacho shughuli za michezo, zilikuwa zimesimamishwa, wachezaji mbalimbali, hasa wa Ligi Kuu Bara, walikuwa wakifanya mazoezi binafsi kulingana na program walizopewa na makocha wao.

Wengi walionekana wakijifua ufukweni, wengine majumbani kwao, ilimradi tu kila mmoja akihakikisha anakuwa fiti ili ligi ikirejea, asiwe kichekesho mbele ya wenzake na wapenzi wa soka kwa ujumla.

Hatimaye ligi hiyo inarejea, hivyo BINGWA tunaona wakati wa kufahamu ni wachezaji gani walikuwa wakijifua hasa na ni wapi walikuwa wakifanya maigizo umewadia.

Kama kila mmoja wetu anavyofahamu, mchezo wa soka ni wa wazi kiasi kwamba mchezaji aliyekuwa akijifua vilivyo au aliyekuwa akitufanyia maigizo, ataonekana tu, tena ndani ya dakika chache za mchezo.

Ukizingatia soka ndio ajira ya wachezaji wetu, kwa mapumziko ya miezi miwili ya kipindi hiki cha corona, litakuwa ni jambo la kushangaza kama itatokea kuna mchezaji ataingia uwanjani na baada ya dakika tano, ulimi nje, kwa maana pumzi kukata na hivyo kuigharimu timu yake.

Akitokea mchezaji kama huyo, hakika hakuna mpenzi wa soka atakayemwelewa zaidi ya kumwona kichekesho na ni wazi hata akizomewa na mashabiki, hakuna atakayelaumu.

Kazi kwenu wanasoka wate, mlichokuwa mkidai mnakisubiri kwa hamu, kwa maana ya tamko la Serikali kurejea michezo, hicho kimetimia, tunasubiri mtuonyeshe kile mlichokuwa mikikifanya kupitia picha na video zenu mlizokuwa mkizituma kwenye mitandao ya kijamii.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -