Friday, November 27, 2020

MIDO FUNDI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

HUSSEIN OMAR NA MARTIN MAZUGWA

SIKU chache baada ya kiungo mchezeshaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, kuhusishwa na kuiacha timu hiyo mwishoni mwa msimu, tayari miamba hao wa soka la Tanzania wamepata kiungo mwingine fundi kuziba nafasi hiyo.

Yanga walikuwa katika harakati nzito za kumnasa kiungo huyo kwa muda mrefu lakini juhudi hizo zilishindikana mara kadhaa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kufikia dau kubwa lililotakiwa na kiungo huyo.

Kwa sasa mabingwa hao watetezi wako katika hatua nzuri ya kukamilisha dili la kumtwaa kiungo Kenny Ali kutoka kwa Mbeya City ya jijini Mbeya.

Mpango wa Yanga wa kumsajili kiungo huyo ambaye juzi aliisumbua sana Simba, umenaswa na BINGWA baada ya kiungo huyo kutua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi yao na Simba  ambapo mabosi wa Yanga walifanya mazungumzo naye kuhusu usajili wake.

“Ni kweli tuna mpango wa kumsajili na hapa tumezungumza naye kwa kuwa mpango huu umekuwepo muda mrefu lakini ulishindikana kutokana na sababu kadhaa hapo mwanzo,” alisema kiungo huyo wa Yanga mabaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini kwa kuhofia kuhusishwa na tuhuma za kuihujumu Simba.

“Nimeongea na Ngassa na Kenny sasa kwa kawaida mwenye hali kama hii, watu wakikuona wanakuhusisha na masuala yasiyofaa ya hujuma, sasa usiandike jina langu, lakini ni ukweli kwamba Yanga inamhitaji Kenny tangu zamani Pluijm alimpendekeza na sasa Lwandamina amemwona na tunampa CD amone na bila shaka atamuona tutakapocheza na Mbeya City, kwa hiyo tumekumbushia,” alisema.

Mabingwa hao watetezi mwaka jana walishindwa kunasa saini ya  kiungo huyo kutokana na kuwa na mkataba wa mwaka mmoja na wagonga nyundo wa Jiji la Mbeya, lakini kitendo cha kufunga na kwenda jukwaa la Yanga kiliibua hisia kwa wapenzi na mashabiki wa Jangwani waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.

Akizungumza na BINGWA jana, Kenny Ali alisema hana tatizo na kujiunga kuwachezea mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, endapo watafuata taratibu za kumsajili yupo tayari kukipiga nao msimu ujao wa ligi.

“Nipo tayari mpira ndio kazi yangu ila tutaongea zaidi kwa kuwa nipo safarini kuelekea Mbeya, nikifika tutachonga zaidi,” alisema Kenny.

Kenny  ndiye kiungo aliyekuwa kikwazo kwa Simba wakati Wekundu hao wa Msimbazi walipovaana  na Mbeya City mwishoni mwa wiki, Uwanja wa Taifa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kuanzia mchezo wa kwanza mjini Mbeya hadi ule wa ugenini Dar es Salaam.

Kwa kipindi kirefu, Yanga imejikuta ikiwa bado na tatizo katika nafasi ya kiungo namba sita kiasi cha kumtumia Justin Zullu ambaye hata hivyo ameshindwa kufanya kile kilichotarajiwa na wengi katika nafasi hiyo pindi akisajiliwa na timu hiyo.

Kwa vipindi tofauti, Yanga imejaribu kuwatumia Said Juma Makapu, Thaban Kamusoko, Mbuyu Twite (ambaye kwa sasa yupo Fanja FC ya Oman) na wengineo kadhaa katika nafasi hiyo ya kiungo mkabaji, lakini wote walionekana kushindwa kuziba pengo hilo lililoachwa na viungo, Athuman Idd Chuji na Frank Domayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -