Thursday, October 29, 2020

Mido hatari atua Yanga

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

*Ni raia wa Angola fundi hasa wa mpira, akipangwa na Tonombe ni balaa

*Mashine mpya zaanza kutambulishwa, kuna watu hawataamini

KIKOSI: Shikalo, Shomari, Mustafa, Mwamnyeto, Lamine, Tonombe, Tuisila, Carlinhos, Yacouba, Junior, Farid

NA ZAINAB IDDY

KIUNGO fundi wa mpira raia wa Angola, Carlos do Carmo, maarufu kwa jina la Carlinhos, ameingia katika anga za Yanga, akitarajiwa kutua Jangwani muda wowote kuanzia sasa.

Habari ambazo BINGWA limezipata jana jioni, zinasema kuwa baada ya Yanga kumkosa Mzambia Larry Bwalya aliyenyakuliwa na Simba, wamepewa jina la Carlinhos wakijulishwa kuwa kiungo huyo ni fundi balaa.

Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, Yanga wameambiwa kwa kuwa wana uhakika wa kumpata Mukoko Tonombe wa AS Vita Club ya DR Congo, ni heri wakamchukua Carlinhos ili kuunda safu hatai ya kiungo.

“Mhandisi Hersi Said alipokuwa Kinshasa (DR Congo), aliambiwa kama tumemkosa Larry, ni heri tukamchukua Carlinhos kwani huyu anaweza kucheza nafasi ya kiungo wa juu kwa kuwa tayari tunaye Mukoko ambaye ni kiungo mkabaji.

“Aliambiwa uzuri wa wote wawili, wanaweza kubadilishana nafasi kwani wanazimudu vema japo Mukoko ni mzuri zaidi kucheza kama kiungo mkabaji, japo pia ni mfungaji mzuri tu na mpishi wa mabao pia,” alisema mtoa habari wetu wa uhakika kutoka ndani ya Yanga.

Juu ya Carlinhos anayekipiga katika kikosi cha G.D. Interclube ya Angola, alisema kiungo huyo Muangalo, mwenye asili ya Ureno, bado ni kijana mdogo mwenye uwezo wa kuitumikia Yanga kwa muda mrefu.

Alisema tayari Mhandisi Hersi ameanza mazungumzo na Carlinhos na kwamba leo itajulikana iwapo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 anayekipiga timu ya Taifa ya Angola, ni mali ya Yanga au la.

Mbali ya Carlinhos, wachezaji wengine wa kigeni waliopo njiani kutua Yanga ni Tuisila Kisinda kutoka AS Vita Club, Tonombe, Muhadjiri Hakizimana (Rwanda), Mghana Michael Sarpong (Rayon Sports, Rwanda) na Sogne Yacouba (Asante Kotoko, Ghana).

Ukiachana na hao, wapo wazawa Kibwana Shomari (Mtibwa Sugar), Yassin Mustafa (Polisi Tanzania), Bakari Mwamnyeto (Coastal Union), Waziri Junior (Mbao) na Farid Mussa aliyekuwa akicheza soka la kulipwa nchini Hispania.

Pia, Wanajangwani hao wamemrejesha kikosini beki wao wa zamani, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ aliyekuwa akisakata kabumbu nchini Marekani.

Kutokana na usajili unaoendelea Yanga hadi sasa, mwelekeo wa kikosi chao cha msimu ujao unaweza kuwa kama ifuatavyo:

Kipa ni Farouk Shikalo, Kibwana Shomari (beki wa kulia), Yassin Mustafa (beki wa kushoto), wakati mabeki wa kati ni Bakari Mwamnyeto na Lamine Moro.

Kiungo mkabaji ni Mukoko Tonombe, wakati kiungo mshambuliaji ni Carlinhos, huku winga wa kulia akiwa ni Tuisila Kisinda na winga wa kushoto ni Farid Mussa.

Washambuliaji wa kati ni Sogne Yacouba na Waziri Junior, huku kwenye benchi kukiwa na wakali wengine kama Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Metacha Mnata, Paul Godfrey ‘Boxer’, Adeyum Saleh, Ramadhan Kabwili, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Mapinduzi Balama na wengineo.  

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -