Friday, October 23, 2020

MIDO MGHANA WA SIMBA ZULU CHA MTOTO

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...
  • Aonyesha mambo ya ajabu Chamazi, mashabiki Simba wapagawa
  • Mkude sasa kujua kama maharage ni mboga au kiungo cha makande

HUSSEIN OMAR NA SAADA SALIM

KIUNGO mpya wa Simba, Mghana James Kotei, jana alionyesha kiwango cha juu cha soka na kumfunika ‘mkata umeme’ wa Yanga, Mzambia Justice Zulu, aliyejinadi kwa mara ya kwanza Jumamosi ya wiki iliyopita katika mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar.

Kotei, aliyetua nchini hivi karibuni ili kuziba pengo la kiungo mzoefu, Jonas Mkude, aliyedaiwa kuidengulia Simba kabla ya kutuliza mzuka Msimbazi, jana kwa mara ya kwanza alichomoza mbele ya mashabiki wa Msimbazi wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar, kwenye Uwanja wa Chamazi Complex na kufanya mambo makubwa.

Zikiwa ni siku mbili baada ya Zulu kuonyesha alichonacho mbele ya mashabiki wa Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Kotei hakuwa na la kupoteza jana, ambapo pamoja na Simba kufungwa mabao 2-0, lakini aliwakosha mashabiki wa Msimbazi kwa soka lake la hali ya juu.

Kotei tangu dakika ya kwanza, alionyesha kujiamini vilivyo, akidhihirisha utaalamu wake katika kukaba, kupiga pasi zinazofika kwa walengwa, tena kwa wakati sahihi, lakini pia kufungua vyumba kuwawezesha wenzake kumpasia pale ilipobidi.

Ukiachana na hayo, Kotei alionyesha utulivu wa hali ya juu, akiwa ni fundi wa kumiliki mpira kiasi cha kuwapa shida wapinzani kumpora, lakini pia akiwa hana papara katika kufanya maamuzi.

Kwa kifupi, Kotei alithibitisha kuwa bora kuliko Zulu, ambaye japo alionyesha uhodari wa kupiga pasi na kufungua vyumba, lakini alishindwa kukonga nyoyo za mashabiki wa Yanga waliojazana uwanjani hapo, akionekana kuwa mzito na hivyo kutokuwa ‘flexible’ (kushindwa kunyumbulika).

Mwisho wa siku, japo wapo watu wa Yanga waliomwelewa wakiamini muda si mrefu ‘watu watamwelewa’, lakini wapo wachache waliombeza wakisema: “Mkata umeme amepigwa ‘shock’ Uwanja wa Uhuru.”

Katika mchezo wa jana, makocha wa Simba kama ilivyokuwa kwa wale wa Yanga, walionekana kutosaka ushindi zaidi ya kuwapima wachezaji wao kwa kila mmoja kupewa nafasi ya kuonyesha alichonacho baada ya mazoezi ya wiki kadhaa, tayari kuuanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unaotarajiwa kuanza wikiendi hii.

Mbali ya Kotei, mchezaji mwingine aliyecheza kwa mara ya kwanza ni kipa Mghana, Daniel Agrey, ambaye alikubali kuruhusu kufungwa mabao mawili na Stamili Mbonde dakika ya kwanza na Japhary Salum (dk 34).

Bao la Simba liliwekwa kimiani na Mohammed Ibrahim dakika ya 36.

SIMBA: Daniel Agrey, Jenvier Bukungu, Mohammed Hussein, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, James Kotei, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Fredrick Blagnoon, Mussa Ndusha na Mohammed Ibrahim.

MTIBWA SUGAR: Said Nduda, Ally Shomary, Hassan Timbe, Henry Joseph, Salim Mbonde, Shaban Nditi, Kelvin Friday, Mohammed Banka, Stamili Mbonde, Jafary Salum na Haruna Chanongo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -