Tuesday, November 24, 2020

MIL. 656 KUSAJILI KIKOSI KIPYA YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY

WAKATI hivi sasa wadau wa soka wakiwa wamekata matumaini ya kutetea taji lao la Ligi Kuu Tanzania Bara, uongozi wa Yanga unatarajia kutumia zaidi ya milioni 656 kwa ajili ya kusajili wanandinga wapya msimu ujao wa ligi na michuano ya Kimataifa.

Kiasi hicho cha fedha kinataraji kutumika kwa ajili ya kusajili wachezaji wapya pekee watakaohitajika na benchi la ufundi chini ya kocha Mzambia, Geogre Lwandamina.

Bajeti  hiyo itafika baada ya Lwandamina kupeleka ripoti yake aliyotakiwa kuiwasilisha na uongozi wa juu yenye uhitaji wa wachezaji watatu wa kimataifa pamoja na saba wazawa ambao idadi hiyo itaongezeka au kupungua baada ya kuzungumza na wanandinga wao waliomaliza mikataba yao iwapo kama watahitaji kuongeza au la.

Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa na BINGWA, kabla ya ripoti hiyo Lwandamina alitakiwa kuwasilisha mapema bajeti yake ya usajili lakini akiwekewa kiwango ambapo kwa wageni wametakiwa wasizidi milioni 150, huku wazawa si zaidi ya milioni 70 kwa mchezaji mmoja.

“Bajeti hiyo ni kwa ajili ya usajili wa wachezaji wapya pekee  lakini itaongezeka kwa kuwa wapo wanaomaliza mikataba yao na mwalimu ameona wanahitajika kubaki na timu hiyo lazima uongozi utakaa nao ili kuzungumza juu ya kuwapa mkataba mpya, hivyo kwa kawaida lazima kunav itu vitaongezeka,” alisema mtoa habari wetu.

Hadi sasa Yanga inauhitaji wa kiungo mkabaji na mchezeshaji pamoja na mshambuliaji mmoja kutoka nje hasa kutokana na ukweli kwamba nafasi ya kiungo mkabaji inayochezwa na Justine Zullu bado haijapata mtu sahihi.

“Kama unavyojua Ngoma yawezekana akaondoka na pia kwa kiungo mshambuliaji Niyonzima (Haruna)  na Kamusoko nao mikataba yao inaisha, hivyo hawajaamua kama watabaki au vipi kwa hiyo kocha ameleta bajeti kwa kuzingatia maeneo hayo matatu ya wachezaji wa kimataifa na tunahitaji wachezaji wa uhakika hasa ili kuwa na kikosi imara,” alisema.

Alisema kuhusu wachezaji wa ndani, tayari kocha huyo ameona wachezaji kadhaa lakini amependekeza kuwe na usajili wa nafasi nne mpya, hasa kutokana na ukweli kwamba baadhi ya wachezaji anatarajia kuwaruhusu waondoke.

“Kwa hiyo kocha ameona kwamba kikosi chake kiongezeke nyota saba wapya, ingawa wanaweza kupungua endapo pengine Niyonzima na Kamusoko wataamua kuendelea maana kocha hana shida na uwezo wao, lakini kwa hawa wa ndani lazima wasajiliwe japo watano,” kilieleza chanzo chetu cha ndani kutoka Yanga.

Bajeti hii ya milioni 656 ni ya awali, hivyo inaweza kuongezeka zaidi na kwamba msimu mpya Yanga inahitaji kuwa na kikosi kizuri zaidi.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, hakuwa tayari kulizungumzia hilo kwa sasa kwa kuwa akili yake imejikita katika maandalizi ya mechi yao dhidi ya MC Alger ya Algeria pamoja na kutetea ubingwa wao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -