Sunday, October 25, 2020

MILLEN MAGESE AMPIGIA SALUTI NAPE NNAUYE

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI wa Kampuni ya Millen Magese Group (MMG), Millen Magese, ameishukuru Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, huku akifurahishwa na uwakilishi mzuri wa Miss Tanzania, Julitha Kabete (19), aliyetinga tano bora katika mashindano ya Afrika.

Julitha aliipeperusha vema bendera ya Tanzania kwa kuingia hatua ya tano bora ya mashindano yaliyofanyika Jumamosi iliyopita nchini Nigeria na kuitoa Tanzania kimasomaso.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Millen alisema ni faraja kubwa kwake na nchi yake kwa Julitha kuingia hatua ya tano bora, lakini sababu kubwa ikiwa ni ushirikiano iliyoupata.

“Napenda kuchukua fursa hii kuishukuru Serikali, kupitia Waziri Nape Nnauye kwa ushirikiano na mwongozo wa kipekee, wazazi na familia nzima ya Julitha kwa malezi yenu kwa binti na kamati nzima ya Miss Tanzania chini ya Mkurugenzi Hashim Lundenga,” alisema Magese.

Kwa upande wake, Julitha alisema kuwa licha kutopata nafasi ya kwanza, lakini ameweza kuiwakilisha vema nchi katika shindano hilo, kwa sababu ushindani ulikuwa mkali sana.

“Kwangu ni faraja kubwa kwa kuwa balozi mzuri wa Tanzania na kuweza kuwashinda wenzangu wengi ikiwamo  mwenyeji wetu ambaye hakuingia katika hatua ya tano kama ambayo mimi nimeipata, nina furaha kubwa sana,” alisema.

Katika shindano hilo, taji lilikwenda kwa Neurite Mendes (23) wa Angola, aliyenyakua kitita cha dola za Marekani 25,000 sawa na Sh milioni 52 na gari jipya (brand new 2016 Ford Escape), safari maalumu ya mafunzo nchini Uingereza na Ubalozi wa Mazingira– Afrika.

Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Refilwe Mthimunye wa Afrika Kusini aliyepata dola za Kimarekani 15, 000, sawa na zaidi ya Sh milioni 32 na Jencey Anwifoje kutoka Cameroon, alishika nafasi ya tatu na kupata dola za Kimarekani 10,000 sawa na zaidi ya  Sh milioni 20.

Kampuni tanzu ya Millen Magese (MMG) imeanzishwa kwa lengo la kuibua, kuinua, kutambua na kukuza vipaji katika Bara la Afrika na ngazi ya kimataifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -