Tuesday, October 27, 2020

MIMI MARS: SIJAWAHI KUKUTANA NA MWANAMUME KING’ANG’ANIZI, WENGI NI WAELEWA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA CHRISTOPHER MSEKEN

KARIBU msomaji wa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi ya kuwauliza maswali watu maarufu katika tasnia ya burudani na leo hii tupo na Marianne Mdee maarufu kama Mimi Mars, msanii anayefanya vyema katika anga la muziki wa Bongo Fleva na wimbo wake Kodoo, karibu.

SWALI: Godbless Mchau wa Kahama anauliza, umefikiria kuunda kundi na dada yako Vanessa Mdee?

Mimi Mars: Hapana, kila mtu ataendelea kufanya kazi zake binafsi kwa sababu naona kama nitakatishwa safari yangu fupi ambayo nimeanza na ninataka niwe na kumbukumbu ya kumwelezea mtu, unajua tukitengeneza kundi mara moja nitakuwa juu na mimi sitaki kubebwa.

SWALI: Hamis maarufu kama Man Chado wa Morogoro, anauliza umejifunza nini muda mfupi ulioingia kwenye muziki?

Mimi Mars: Nimejifunza kujiamini, nilikuwa najichukulia poa sana kwa sababu muda mwingine nilikuwa nakutana na changamoto lakini mwisho wa siku nikajua ninavyozidi kufanya shoo na wasanii wakubwa na kukutana na mashabiki zangu nafarijika na kuzidi kujiamini.

Pia nimejifunza kuweka nguvu katika kusukuma kazi zangu, zamani nilikuwa najua nikiwapa wasanii wenzangu tu inatosha lakini sasa hivi mimi mwenyewe nashughulika.

SWALI: Saidi Makomba wa Tanga Mjini anauliza, huwa unafanya jambo gani kabla hujatumbuiza?

Mimi Mars: Kitu cha kwanza huwa namwomba Mungu ndiyo mambo mengine yanafuata.

SWALI: Martha Immanuel wa Arusha anataka kujua kama una mpango wa kutoa albamu.

Mimi Mars: Mungu akijaalia inaweza kutoka Desemba humo ndani itakuwa na ngoma kali sana na itakuwa na utofauti kidogo.

SWALI: Regina Mgawa wa Vingunguti Dar es Salaam, anauliza ukiwa kama mtunzi wa nyimbo, je, ni wasanii gani umewaandikia nyimbo?

Mimi Mars: Nikihisi nimefika ‘levo’ nzuri ya kumwandikia mtu nitaandika ila kwa sasa hivi kumwandikia mwingine sidhani, mimi ni mwandishi wa nyimbo ambaye bado mchanga ndiyo maana huwa nawashirikisha watunzi kama Young Lunya, Mario na wengine.

SWALI:  Juma Mustafa wa Kinondoni anauliza, ukiwa kama msanii mrembo wa kike unakabiliana vipi na changamoto za kutongozwa?

Mimi Mars: Ninachoshukuru watu wengi wanaonifuata wakitaka tuwe wapenzi huwa nawaeleza kuwa sipo tayari kwa muda huo na huwa wanaelewa sijawahi kukutana na wanaume ving’ang’anizi.

SWALI: Lucas Kushembe kutoka Mwanza anauliza, kwanini umeamua kufanya muziki wa Zouk zaidi na si RnB au miziki mingine?

Mimi Mars: Naimba muziki huu wa kukimbia kwa sababu ni muziki ambao watu wengi wanaupenda, ukiwa klabu, ukiwa kwenye shoo unaona kabisa mashabiki wanapenda nyimbo za kukimbia.

SWALI: Shukuru Moyo wa Coco Beach, Mtwara, anauliza huwa unafanya nini ukipanda jukwaani halafu watu wasishangilie?

Mimi Mars: Imewahi kunitokea, nilikuwa jukwaani lakini mambo hayakuwa vile ambavyo nilipanga, basi nikakomaa tu nikamaliza nikashuka huwa najisikia vibaya.

SWALI: Elisha Leonard kutoka Dodoma, anauliza mwanamume mwenye tabia ipi huwezi kuwa mpenzi wake?

Mimi Mars: Mwanaume anayeongea sana.

Endelea kutuma maswali kwa mchekeshaji Anko Zumo na mwanawe Mai Zumo kupitia namba hapo juu kwa ajili ya wiki ijayo, meseji tu

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -