Wednesday, October 28, 2020

MIMI NIMEMWELEWA HIVI HAZARD

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA KELVIN LYAMUYA

EDEN Hazard ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu England kwa sasa. Kwenye orodha ya wafungaji, anaongoza na mabao yake saba.

Kwenye takwimu za kupiga mashuti, pia hakosekani katika 10 bora akiwa amejaribu mashuti 23 na 10 kati ya hayo akiwa ameyalenga golini, hivyo unaweza kuona ni jinsi gani alivyokuwa imara chini ya Maurizio Sarri.

Huyo ndiye Hazard ambaye msimu wa 2015/16 aliumaliza akiwa na mabao sita tu. Katika msimu mzima wenye mechi zaidi ya 30, Hazard umjuaye alifunga idadi hiyo ya mabao akiwa na jezi ya Chelsea.

Kwa kuweka kumbukumbu sawa, huo ndiyo ulikuwa msimu ambao Chelsea ilimtimua kazi Jose Mourinho baada ya kushindwa kutetea taji la Ligi Kuu England na kuwaachia nafasi Leicester City kuandika historia mpya.

Mourinho alijikuta akipoteza kibarua chake huku Cesc Fabregas, Hazard na Diego Costa wakidaiwa kuwa walimsaliti Mreno huyo. Katika zama za giza totoro pale Stamford Bridge, jamii ya Chelsea ilikuwa nyuma ya Mourinho na mchezaji mmoja tu, Willian.

Takwimu za ‘wasaliti’, Hazard, Costa na Fabregas zilikuwaje hadi kufikia mwishoni mwa msimu mbovu wa bingwa mtetezi, Chelsea na pia mwisho mchungu wa Mourinho.

Hazard alifunga mabao sita na kutoa pasi saba za mabao katika michuano yote. Costa alitikisa nyavu mara 16, pasi nane za mabao na Fabregas alifunga mara sita na kutoa pasi nane za mabao.

Jumla Hazard, Costa na Fabregas walichangia mabao 51 kati ya 91 ambayo yalifungwa na timu nzima ya Chelsea katika michuano yote msimu huo wa 2015/16. Takribani asilimia 56.

Kiwango cha Willian kilikuwa ni cha kuridhisha kwa kuzingatia daraja la ubora wake. Mbrazil huyo alipachika mabao 11 na kutoa pasi saba za mabao katika michuano yote.

Nikagundua kwamba jamii ya wanazi wa Chelsea ilikuwa na haki ya kuwashukia akina Hazard kwa sababu takwimu zao msimu huo hazikulingana na ubora waliokuwa nao.

Msimu huo Costa alikuwa ndiye mfungaji bora wa klabu katika ligi. Nyuma yake akafuatia Willian. Fabregas alimaliza na pasi nyingi za mabao akilingana na Willian.

Hazard naye alitoa pasi za kutosha za mabao lakini alilingana na Willian. Kwahiyo wale wote ambao walikuwa nyuma ya Mourinho alipofukuzwa na kuwagueukia nyota hao watatu, walikuwa na haki hiyo.

Wachezaji wa Chelsea ambao walipaswa kupambana kwa ajili  ya kuinusuru klabu na aibu ya msimu, hawakufanya hivyo. Na ukweli wanaujua kabisa. Ndio maana Hazard ameamua kujiweka huru na kuwa mkweli kwamba alimwangusha mno Mourinho msimu ule.

Ukweli unaouma ndio ambao unamweka mtu huru. Leo hii Hazard amekuwa mtu huru. Amesema ukweli mchungu. Amemuomba radhi Mourinho kwa kufunga mabao sita msimu mzima. Ni wazi kocha huyo pia alikuwa na haki ya kunung’unika suala la usaliti katika kambi yake.

Hazard anapoibuka na maoni yake ambayo kimsingi ni ya kuheshimiwa, kwamba anataka kufanya kazi tena na Mourinho, inabidi utulize akili umwelewe amemaanisha nini.

Wewe pia unaweza ukawa umemwelewa. Nami nimemwelewa vizuri. Tukiungana tunaweza tukamwelewa Hazard kuliko Mourinho atakavyomwelewa mchezaji wake huyo wa zamani.

Kwanza kabisa, Mourinho ataendelea kuwa kocha mwenye mafanikio ya kuheshimika katika historia ya soka na ndio maana huwezi kusikia wachezaji ambao walipata mafanikio chini yake wakimzungumzia vibaya. Siku zote kinacholaumiwa ni mbinu zake.

Lakini heshima katika jina la Mourinho ni lazima iwekwe. Paul Pogba hana kosa lolote kulaumu mbinu za kocha wake, lakini kama angegusa nyeti za Mourinho, ni lazima mtifuano ungekuwa mkubwa sana.

Kwa mwanasoka aliyekomaa katika mchezo huo, huamua kubadili lawama na kuvifanyia vitendo vile vitu ambavyo anahisi havipo sawa. Kuna uwezekano mkubwa kuwa Mourinho na Pogba hawana ugomvi mkubwa sana kama ambao umekuwa ukiripotiwa.

Nina uhakika wa kutosha kwamba mgogoro uliopo baina ya wawili hao ni mitazamo ya mbinu za soka kama vile ilivyotokea katika klabu nyingine alizowahi kuzinoa kama vile Real Madrid.

Hazard alipomwomba msamaha Mourinho, ni kwamba alijutia kiwango kibovu alichokionesha msimu wa 2015/16. Alikiri kuna uzembe mkubwa aliufanya na kushindwa kuonesha kiwango bora.

Historia kubwa ya Mourinho inategemea wachezaji walio tayari kucheza soka uwanjani na si mdomoni. Na ndio maana ili kuilinda heshima yake, Hazard ameibuka na kuilinda pia historia kubwa ya Mourinho.

Aidha, Hazard anaendeleza tu kile ambacho Zlatan Ibrahimovic alikisema siku chache zilizopita kuwa Mourinho bado ndiye kocha sahihi kwa Man United, huku akisisitiza kama wachezaji hawachezi katika kiwango kinachotakiwa, hawezi kufanya miujiza.

Mfano mzuri tutumie kauli aliyoisema Pogba mwezi uliopita kwamba, angependa kuiona Man Utd ikishambulia zaidi kuliko kujilinda. Mourinho amekuwa akiamini tofauti ingawa bado timu yake hufunga mabao na kushinda mechi.

Kiu kubwa ya wanazi wa Man Utd imekuwa ni kuiona timu yao ikicheza soka maridadi, halikadhalika wachezaji nao wanahitaji kuliona hilo. Vyote hivi hawezi kuvifanya Mourinho peke yake, anawahitaji wachezaji wake nao wachangie nguvu yao.

Kwanza tujiulize swali, wachezaji wote wa Man Utd hawawezi kucheza soka la burudani ukiacha mbinu ambayo Mourinho anawapa ya kuhakikisha lango lao halishambuliwi?

Kwa utajiri wa wachezaji wenye vipaji vya soka uliopo Man Utd, naamini wote wale wanao uwezo wa kutoa burudani kila wikiendi iwe Old Trafford ama katika viwanja vya ugenini.

Pogba, Juan Mata, Anthony Martial na wengineo wana uwezo mzuri tu wa kuifanya United iwe tishio katika umiliki wa soka, kutengeneza mashambulizi makali. Kiujumla wanao uwezo wa kuifanya timu hiyo iwe tishio kila kona.

Lakini kwa jinsi wanavyocheza kila wikiendi, inaonekana kama vile wanamsaliti na kuibua hali ya hewa iliyowahi kutokea Chelsea ambayo Mourinho alishindwa kuihimili na kujikuta akitimuliwa.

Sidhani kama Mourinho ni binadamu mwenye nguvu zaidi ya kufanya kazi zaidi ya uwezo wa kimbinu, hivyo kwa kauli ya Hazard ya kusema anataka kufanya kazi na kocha huyo, anamaanisha wachezaji wa Utd hawana budi kujitoa kwa moyo wote.

Tazama historia ya Mourinho akiwa Porto, Inter Milan na hata Chelsea ile ile ya 2014/15, zilikuwa ni timu bora zilizokuwa zikicheza soka safi na vilevile zikiheshimu mbinu ya Mourinho.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -