Wednesday, October 28, 2020

MISS TANZANIA 2018 KUVAA TAJI LA ‘WEMA SEPETU’

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA JEREMIA ERNEST


MREMBO atakayefanikiwa kuibuka kidedea katika fainali za Miss Tanzania 2018, anataarajiwa kuvishwa taji (crown) yenye thamani ya shilingi milioni sita pamoja na gari.

Taji hilo lililotambulishwa katika mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, ni la duara ambalo kwa mara ya mwisho, liliwahi kuvaliwa na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serene walikoweka kambi warembo waliotinga fainali za shindano hilo, Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basila Mwanukuzi, alisema kuwa taji hilo limetengezwa nchini Marekani.

“Crown (taji) hii imetengenezwa nchini Marekani, lina madini ndani yake, likiwa na thamani ya shilingi milioni sita.

“Ninaposema hii ni Miss Tanzania mpya, ninamaanisha ndio maana ninajaribu kutengeneza utofauti na miaka iliyopita,” alisema.

Alisema kuwa warembo wanaoshiriki fainali za shindano hilo mwaka huu, watakaa kambini kwa wiki mbili kabla ya kinyang’anyiro kitakachofanyika Septemba 8, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Basila ambaye ni Miss Tanzania 1998, alisema kuwa warembo hao watakuwa wakinolewa na mwalimu Ben Massai, huku upande wa dansi wakipigwa msasa na Salim Makuka ‘Sammy Cool’.

Juu ya suala zima la majaji wa fainali za mwaka huu, Basila alisema kuwa mashabiki wa urembo wasiwe na wasiwasi na hilo kwani amejipanga kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mshiriki.

“Majaji majina yao yameshapelekwa Basata (Baraza la Sanaa la Taifa), wao ndio wanapitia CV (wasifu) zao baada ya hapo watachagua majina na kuyarudisha katika Kamati ya Miss Tanzania.

“Idadi ya majina tunayotegemea kurudi ni kati ya matano, saba, tisa au 11, namba ambayo haigawanyiki. Basata ndio watakaoamua kulingana na vigezo vinavyokubalika na Miss World kwa kuwa Miss Tanzania ipo chini ya Miss World,” alisema.

Kuhusiana na tiketi za kiingilia cha shoo ya fainali, Basila alisema kuwa wameboresha utaratibu ambapo safari hii zitauzwa kwa njia ya mtandao.

Jumla ya warembo 20 kutoka kanda sita, waantarajiwa kuchuana katika uzuri wa sura, umbo, uelewa, kujiamini, miondoko na mengineyo kumpata Miss Tanzania 2018.

Shindano la Miss Tanzania lilioanza rasmi mwaka 1967, kwa sasa linaratibiwa na Kampuni ya The Look chini ya Basila, aliyelitwaa kutoka kwa Hashim Lundenga na Kampuni yake ya Rino International Agency.

Lundenga aliamua kuachana na shindano hilo kwa hiari yake ili kupisha mwandaaji mwingine, lengo likiwa ni kutoa fursa ya mawazo na mtazamo mpya ili kukiendeleza kinyang’anyiro hicho nyenye mvuto wa kipekee, kikitoa fursa kwa wasichana wa kitanzania kutimiza ndoto zao katika urembo.

Warembo wanaowajia taji la Miss Tanzania mwaka huu ni Pili Matambile (23), Halima Kopwe (19), Nelly Kazikazi (22), Khadija Rutunga (22), Amne Mkwanda (20), Teddy Michael Mkenda (22), Sheyla Msira (20), Adilla Chigomello (22), Sharon Headlam (19), Miriam Mmary (21) na Zuhura Abdul (21).

Wengine ni Nancy Matta (24), Asila Mushi (18), Sandra Giovinazzo (21), Gladness Benson (19), Azama Mashango (22), Florida Venance (23), Linda Mhela (22), Queen Elizabeth Makune (22) na Osmunda Mbeyela (23).

Mafanikio ya juu ya Tanzania katika shindano la Miss World yalipatikana mwaka 2005 pale Nancy Sumari alipofanikiwa kutwaa taji la Mrembo wa Afrika wa Dunia (Miss World Africa).

 

 

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -