Wednesday, November 25, 2020

Miss TZ, Diana Edward humwambii kitu kwa Masanja Mkandamizaji

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA BEATRICE KAIZA

KAMA nilivyoahidi nyinyi watu wangu wa nguvu ndivyo nilivyofanya, nimefanikiwa kumnasa mrembo, Diana Edward ambaye ni Miss Tanzania 2016.

Ikumbukwe kwamba ushindi wa mrembo huyu ulizua mjadala miongoni mwa jamii ya Watanzania, kubwa likiwa utata wa  umri na elimu yake.

Miss huyo amekata kiu ya Watanzania na mashabiki wa urembo kwa kueleza ukweli wa mambo juu yake.

Baada ya kukutana naye na kumwasilishia maswali yenu pamoja na ushauri, haya ndiyo majibu yake;

Swali: Naitwa Bestitudes Mjuni wa Tanga, Diana mwaka huu umefanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania 2016, hongera sana, Watanzania wategemee nini kutoka kwako?

Jibu: Asante kwa pongezi, Watanzania wategemee mabadiliko katika sekta ya urembo, kwani nimejipanga kufanya vitu ambayo vitakuwa tofauti na mamiss waliopita, ikiwemo kufanya vizuri zaidi kimataifa.

Swali: Mama Atu wa Kawe, Dar es Salaam na Rajab Balali wa Kondoa, wanaomba kujua historia kwa ufupi ya Diana tangu alipozaliwa hadi kufikia kushiriki mashindano ya urembo na kushinda.

Jibu: Hili swali nimekutana nalo kila kona na leo naomba Watanzania waelewe kuhusu mimi.

Jina langu kamili naitwa Diana Edward Loi Lukumay, nimezaliwa mwaka 1998 katika Hospitali ya Mount Meru mkoani  Arusha, kabila yangu ni Mmasai.

Elimu yangu ya msingi niliipata kuanzia mwaka 2005-2011, baadaye nilijiunga na Shule ya Sekondari ya Levolosi, kisha Arusha Day kuanzia mwaka 2012-2015.

Matokeo yangu ya kidato cha nne nilipata  daraja la pili (Division two).

Nilichaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano mchepuo wa sanaa katika Shule ya Wasichana ya Bwiru ya  jijini Mwanza, nilikuwa tayari katika tasnia hii ya urembo niliamua kusomea mambo hayo. Kwa kuwa ratiba ya masomo iliingiliana na ile ya mashindano ya Miss Tanzania, nililazimika kuahirisha masomo.

Nilishiriki mashindano ya urembo  katika ngazi ya vitongoji kisha nikajiunga na kambi ya Miss Ubungo 2016-2017 ambapo nilishiriki na kushika nafasi ya tatu.

Baada ya kuahirisha masomo yangu kwa muda, niliomba kujiunga na Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM) kwa ajili ya kusomea mambo ya kodi.

Wakati  masomo yanaanza tayari nilikuwa katika kambi ya Miss Tanzania, hivyo nililazimika kuahirisha kwa muda. Hii ndiyo historia yangu fupi.

Ushauri: Naitwa Haruna Mtwale wa Masumbwe Geita, ushauri wangu kwa Diana naomba  ufate  kanuni na taratibu za mshindano ya Miss Dunia ili uweze kufanya vizuri.

Jibu: Asante kwa ushauri mzuri na mimi naomba Mungu niweze kutimiza ndoto yangu ya kurudi na taji la Dunia.

Ushauri: Naitwa Octavian Sango wa Mwananyamala, Dar es Salaam. Dada Diana kwenye mafanikio lazima ziwepo changamoto, Mungu amekusaidia mpaka ukaibuka Miss Tanzania 2016, jambo la muhimu zidisha maombi kwa Mungu ili uweze kutimiza ndoto zako.

Jibu: Asante sana Octavian kwa ushauri mzuri.

Swali: Naitwa Baba Idd wa  Dar es Salaam. Swali langu kwa Diana kwenye shindano la Miss Kinondoni ulikuwa mtu wa ngapi.

Jibu: Katika shindano la Miss Kinondoni nilikuwa mshindi wa kwanza na lilifanyika Sinza.

Swali: Naitwa Yusuph Omary wa Kigamboni, je, akinyang’anywa taji kwa sababu ya skendo ambazo zinaenea kwenye mitandao ya kijamii ni kitu gani atafanya?

Jibu: Maneno yanayoongelewa katika mitandao ya kijamii kuhusu mimi hayana ukweli na kama ikitokea kunyang’anywa taji nitamshukuru Mungu, kwani kila jambo linalomkuta binadamu linakuwa na sababu.

Swali: Naitwa Amiri Shamra wa Mbeya, naomba kujua Diana ni mtoto wa ngapi katika familia ya mzee Edward?

Jibu: Mimi ni mtoto wa tatu katika familia ya  watoto wa nne.

Swali: Naitwa  Ramadhani wa Zanzibar, kitu gani au mbinu zipi alizitumia hadi akafanikiwa kuwashinda mamiss wengine 29?

Jibu: Kikubwa ambacho kimenifanya niwe Miss Tanzania ni kujiamini na kumtegemea Mungu kwa kila jambo, kwa kuwa yeye ndiye mwokozi,p ia kuwaheshimu wakubwa na wadogo.

Swali: Naitwa Abeid Kibuga, mimi si mpenzi wa mambo haya ya urembo, ila mwaka huu nilijikuta nikifuatilia hadi mshindi alipopatikana ambaye ni Diana. Swali langu kwa miss wetu, kitu gani hasa kilikufanya ukawapa kipaumbele Wamasai  na kuwa na kaulimbiu ya Masai dondosha wembe?

Jibu: Niliona Wamasai bado wanateseka na suala la ukeketaji na lengo langu ni kuwasaidia wasichana wanzangu. Kuhusu  kaulimbiu ya Masai dondosha wembe haitaishia hapo bali itaendelea kwa makabila mengine.

Swali: Naitwa Sara Tesha wa Moshi, Diana una kipaji gani tofauti na mambo ya urembo?

Jibu: Mbali ya  urembo, nina kipaji cha kuigiza.

Swali: Naitwa Eva Mpanju wa Dar es Salaam, Diana unampenda msanii gani wa kiume hapa Tanzania?

Jibu: Nampenda Masanja kwa sababu ni kijana mcha Mungu.

Swali: Naitwa Erick Samweli wa Dar es Salaam, naomba kujua Diana ‘instagram’ anatumia jina gani?

Jibu: Instagram natumia Dianaflave.

Hawa ni baadhi ya wapenzi wa Miss Tanzania, Diana Edward, waliojitokeza kumuuliza maswali pamoja na kumpa ushauri.

Katika toleo lijalo tunamleta kwenu mcheza filamu mahiri nchini, Salim Mohamed kama Gabo.

Filamu yake iliyotoka hivi karibuni inajulikana kama ‘Safari ya Gulo’.

Tumia fursa hii kumuuliza maswali ili kukata kiu yako lakini pia unaweza kumpa ushauri kwa kutuma sms kupitia namba ya simu iliyoko hapo juu na majibu yatapatikana hapa hapa katika toleo la Jumanne ya wiki ijayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -