Tuesday, November 24, 2020

MIUJIZA INAENDELEA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Leicester, England

Leicester City wameongeza ukurasa mwingine kwenye kitabu chao cha miujiza kwa kuwatoa Sevilla na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza.

Kufuatia hatua hiyo, ni ngumu kuitoa klabu hiyo kwenye uwezekano wa kufanya muujiza mwingine wa kunyakua ubingwa wa michuano hiyo kama ilivyokuwa Ligi Kuu England msimu uliopita.

Real Madrid na Barcelona nao wametinga robo fainali. Bayern Munich, Juventus na Borussia Dortmund wanaungana na klabu hizo za Hispania.

Kocha wa muda wa klabu hiyo ya Leicester, Craig Shakespeare, aliendelea na utamaduni wake wa kupanga kikosi cha kwanza kilichoipa ubingwa timu hiyo kwa mara ya tatu mfululizo na wamefanikiwa kushinda michezo yote.

Habari iliyozagaa ni kwamba wachezaji wa Leicester wamemsaliti kocha wao wa zamani Claudio Ranieri, ambaye ametimuliwa wiki iliyopita. Kuna uwezekano wa hilo kuwa ni kweli kwamba wachezaji walimsaliti Ranieri hasa ukiangalia kiwango wanachokionyesha sasa.

Baada ya kuibuka kwao na kunyakua taji la ligi kuu, wengi walitarajia kuwaona wakishuka daraja, lakini mambo yamekuwa tofauti baada ya Wes Morgan na wanzake kufanya kazi kubwa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Shakespeare amefanikiwa kuwarudisha wachezaji wote pamoja na wao wakaonyesha uwezo wao na Sevilla walikiona cha moto.

Safu ya ulizi ya Leicester ilicheza kwa nidhamu na kiungo mkabaji Wilfred Ndidi, alifanya kazi kubwa ya kuwalinda. Marc Albrighton aliongeza nguvu na Shinji Okazaki alionekana kila sehemu. Huku Jamie Vardy akiisumbua safu ya ulinzi ya Sevilla, huku kikosi hucho cha Leicester kikionekana hatari kwenye mashambulizi ya kushtukiza.

Baada ya Shakespeare kumtoa Okazaki ilionyesha Leicester wamerudi kwenye zama zao. Hata Riyad Mahrez alikuwa akifanya kazi, alikaba sana kipindi cha kwanza zaidi ya wachezaji wenzake. Mpira wake wa adhabu ndio ulizaa bao la kwanza lililofungwa na Morgan kabla ya Albrighton kuongeza bao la pili kwa mguu wa kushoto. Penalti ya Steven N’Zonzi ilikuwa ni ya pili kudakwa na mlinda mlango Kasper Schmeichel katika hatua hiyo ya mtoano na hilo halikuwa jambo la kushangaza kutokea Leicester.

Vardy amekosolewa na mchezaji wa zamani wa Manchester United, Gary Neville kwa kumsababishia Samir Nasri kadi nyekundu.

Ukichana na majanga hayo waliyoyapata Sevilla kwenye uwanja huo wa King Power, nao Manchester City na Liverpool walipokea vichapo kwenye mechi za Ligi Kuu England.

Shakespeare, ni kocha watatu wa England kuweza kuvuka hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku hajajitoa kwenye uwezekano wa kunyakua taji hilo.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -