Tuesday, November 24, 2020

‘MIZINGA’, GONJWA LINALOWATESA AKINA DADA WA KILEO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MICHAEL MAURUS

KARIBUNI wapenzi wasomaji wa safu hii ya mahusiano ambayo huwajia kila Jumamosi na Jumanne, ikilenga kufahamishana hili au lile kuhusiana na mambo ya mapenzi, wengine wakiita mahaba.

Kwanza nitoe shukrani zangu kwa wote ambao wamekuwa wakiwasiliana nami kwa njia mbalimbali, aidha wakiuliza au kutoa maoni kuhusiana na safu hii.

Baada ya salamu hizo, nigeukie mada ya leo ambayo inahusiana na ‘makosa ambayo wenza wamekuwa wakiyafanya na mwisho wa siku kujikuta wakihatarisha mahusiano yao.

Ndugu msomaji, bila shaka unaweza ukawa umesikia kama si kuona uchumba au uhusiano wa wawili waliopendana ukivunjika baada ya muda mfupi.

Tena inawezekana hilo limetokea baada ya mbwembwe za kila upande kila mmoja akijinadi kupata mtu sahihi anayeamini ndiye anayeweza kuanzisha naye familia.

Lakini ghafla bin vuu, unasikia au kuona wale waliokuwa wakitamba mbele ya wenzao kupata wapenzi walioingia mioyoni mwao, wanaishia kujilaumu ‘kuingia mkenge’.

Kati yao, wapo ambao huwa tayari kuanika sababu za kuvunjika kwa mahusiano yao, wakati wengine wakibaki kuumia moyoni.

Ni kutokana na hilo, leo nimeona ni vema kuwaletea sababu zinazosababisha kuvunjika kwa mahusiano baina ya wawili waliopendana ndani ya muda mfupi.

Sababu ni nyingi hasa, lakini kwa leo ninaitaja moja tu ambayo ni ‘mizinga’ kama inavyofahamika na wengi, zaidi wakiwa ni wanaume.

Hili linawahusu wasichana zaidi ambapo wamejikuta wakiwapoteza hata wale waliokuwa na nia nao ya dhati kabisa ya kuanzisha nao uhusiano wa kudumu kutokana na kushindwa kujizuia na kuanza kuwalilia shida wapenzi wao muda mfupi baada ya kufahamiana.

Unaweza kukuta binti amefahamiana na mvulana fulani na siku hiyo hiyo baada ya kuachana, anamtumia sms: “baby naomba unisaidie au uniazime Sh 10,000/50,000 kwa tigopesa, nina shida sana, help me (nisaidie) mpenzi wangu.”

Kwa mwanaume ambaye ana nia ya dhati na msichana huyo, anaweza kumtumia msichana huyo fedha alizoombwa au asimtumie na kisha kuingia mitini moja kwa moja kiasi cha kushindwa hata kupokea simu au kujibu sms za msichana husika.

Wasichana wengi wamekuwa wakiingia kwenye mtego huu hasa kwa zama hizi ambazo maisha yamekuwa magumu mno. Wakati mwingine wanajikuta wakitembea wakiwa na mawazo lukuki kutokana na shida zinazowakabili kiasi kwamba anapojitokeza mwanaume yeyote na kumwambia ‘I love you (nakupenda), humwona kama ndiye mkombozi wa matatizo yake. Hilo ni kosa kubwa sana wanalolifanya akina dada wa siku hizi.

Kwa bahati mbaya wanapofanya hivyo dhidi ya mwanaume aliyepanga kuwa naye kwa muda mrefu na si ‘kupita’ tu, hujikuta akipoteza bahati yake na kuishia kulalama ‘wanaume wa siku hizi ni bahili hatari’.

Akina dada wanatakiwa kufahamu ni kosa kubwa sana kumpiga mzinga mtu uliyefahamiana naye ndani ya muda mfupi hata kama una shida kiasi gani, ni heri ikiwezekana ulale na njaa hata kwa siku tatu kuliko kumwomba fedha mwanaume aliyekutongoza ndani ya muda mfupi, iwe ni saa, siku au wiki chache zilizopita. Labda kama huna mpango naye bali unataka kumlia vyake tu halafu uendelee na hamsini zako.

Unapompiga mzinga mwanaume aliyeonyesha nia ya kujenga uhusiano wa kimapenzi nawe, tafsiri yake ni kwamba wewe (mwanamke) huna staha na ni dalili ya tamaa na kukosa uvumilivu hata pale unapokuwa naye kiasi kwamba ukiwa na shida, haitakuwa kazi kwako kutoka nje (kumsaliti) ya mpenzi wako ili kupata msaada.

Kwa leo tuishie hapo, tukutane Jumanne ya wiki ijayo ambapo nitawaletea mada nyingine kali.

Kama una lolote la kuchangia juu ya mada hii, tuwasiliane kupitia simu namba 0713 556022 au anuani pepe: michietz@yahoo.com.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -