Thursday, November 26, 2020

MKATIENI TIKETI MAPEMA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Yanga watamba Nov 7 kuna mtu atatupiwa virago Simba

Wasisitiza pointi tatu kwa Gwambina, wawapa ‘home work’ mashabiki 

NA MWANDISHI WETU

YANGA wamerusha kombora Simba, wakiwataka watani wao hao wa jadi, kumkatia tiketi Kocha Mkuu wao, Sven Vandenbroeck kwani wana uhakika baada ya dakika 90 za mchezo baina yao Jumamosi hii, Mbelgiji huyo atatupiwa virago vyake.

Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana siku hiyo katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Tayari homa la pambano hilo imeanza kupanda kwa timu zote hizo, kila moja ikipanga mikakati ya kuibuka na ushindi ili kuwapa raha mashabiki wao.

Ukiachana na suala zima la pointi tatu, ushindi baina ya timu hizo kongwe hapa nchini, una maana kubwa kutokana na utani wa jadi uliopo kati yao.

Hata hivyo, Yanga ndio wanaoonekana kuwa na presha zaidi ya kushinda ili kulipa kisasi cha kufungwa mabao 4-1 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports, hatua ya nusu fainali msimu uliopita.

Kwa upande wa Ligi Kuu Bara, Yanga ndio wenye rekodi ya kujivunia kwani msimu uliopita, walivuna pointi nne kati ya sita kutoka kwa watani wao hao baada ya kupata sare ya mabao 2-2 mzunguko wa kwanza, kabla ya kushinda bao 1-0 waliporudiana.

Utamu zaidi katika mchezo wa Jumamosi, ni kutokana na hali ya timu hizo katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga wakiwa wamewaacha Simba kwa pointi sita.

Timu zote zikiwa zimecheza mechi nane, Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 22, wakati Simba wanakamata nafasi ya tatu na pointi zao 16.

Kutokana na hali hiyo, Simba watakuwa wakipania zaidi kuifunga Yanga Jumamosi ili kupunguza pengo la pointi kama moja ya mkakati wao wa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa nne mfululizo.

Kwa kufahamu hilo, Yanga wameibuka na kutamba kuwa watani wao hao wa jadi, wasitarajie ushindi Jumamosi zaidi ya kipigo.

Akizungumza na BINGWA jana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema kuwa moto wao waliouwasha wataendelea nao katika kila mechi, ikiwamo Jumamosi dhidi ya Simba hadi watakapotangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2020/21.

Alisema kuwa baada ya kukusanya pointi sita Kanda ya Ziwa kwa kuzichapa KMC na Biashara United, wamebakiza pointi nyingine tatu dhidi ya Gwambina na baada ya hapo, wataelekeza nguvu zao kuelekea mchezo wa Jumamosi.

Alisema kuwa kwa kikosi chao cha sasa, umoja na mshikamano baina ya wachezaji, viongozi na wanachama wao, hakuna kitakachowazuia kutwaa ubingwa msimu huu.

“Mkakati wetu wa kwanza ndani ya wiki hizi mbili, ilikuwa ni kuchukua pointi tisa Kanda ya Ziwa, tayari tumechukua sita bado tatu dhidi ya Gwambina ambazo nazo tutazipata tu.

“Baada ya hapo, tutaanza kumuwinda ‘mnyama’ (Simba). Niwahakikishie wapenzi wa Yanga lazima tutamfunga tu Simba kwani kikosi chetu cha sasa kipo vizuri. Kama tuliweza kuchukua pointi nne msimu uliopita na kikosi kile, unadhani itakuwaje kwa Yanga hii ya sasa?

“Ninachopenda kuwaambia Simba, wamkatie tiketi mapema kocha wao, Sven kwani Jumamosi ndio mwisho wake, lazima atafukuzwa tu baada ya kumfunga maana tumesikia tukiwafunga wanamfukuza kocha wao, hivyo waende wakamkatie tiketi mapema wasije wakachelewa na kukuta zimeisha,” alitamba Mwakalebela.

Mwakalebela aliyewahi kushika wadhifa wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) anayelifahamu vema soka la Tanzania, aliwashukuru wachezaji wao kwa kuipigania timu yao, lakini pia akiwamwagia sifa mashabiki ambao wamekuwa pamoja na timu kila inapokwenda kucheza kuhakikisha ushindi unapatikana.

“Pamoja na ubora wa kikosi, ushindi mfululizo tunaoupata pia umechangiwa na sapoti ya mashabiki wetu, tunawaomba waendelee na moyo wao huo huo kwani wao ni sehemu muhimu ya mafanikio ya Yanga,” alisema.

Pamoja na kuwa kwenye nafasi ya pili, Yanga imelingana pointi na virana Azam ambao wamecheza mechi tisa, wakati Wanajangwani hao wakishuka dimbani mara nane.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -