Saturday, October 31, 2020

MKAZI WA SENGEREMA AKABIDHIWA BAJAJI YA SPORTPESA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU

MKAZI wa Sengerema jijini Mwanza, Mayala Mabula (30), amekabidhiwa zawadi yake ya bajaji aliyoshinda kupitia promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa inayoendeshwa na Kampuni ya Kubashiri ya SportPesa.

Mabula ambaye ni mshindi wa droo ya nane, alikabidhiwa zawadi yake hiyo ya bajaji juzi akiungana na washindi wengine walioibuka kidedea baada ya kubashiri michezo mbalimbali ya soka kupitia SportPesa.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi yake hiyo, Mabula alisema  aliupokea ushindi huo kwa furaha ya aina yake, huku akielezea jinsi alivyopagawa baada ya kuona timu ya SportPesa imetoka Dar es Salaam mpaka mkoani Mwanza kumkabidhi bajaji yake mara baada ya kushinda.

“Hakuna siku nimefurahi kama leo (juzi), wakati naanza kucheza na SportPesa kutumia simu yangu ya mkononi kwa kupiga *150*87#, nilidhani ningeshinda pesa (fedha) pekee, niliamini hivyo maana sikudhani kama huu mchongo wa bajaj ni kweli, nilijua labda wanapewa watu wa Dar es Salaam, kumbe yeyote anayecheza anaweza kushinda. Ama kweli sasa nimeamini kumbe ni kweli jamani,” alisema Mabula.

Mshindi huyo alisema tangu ameanza kucheza na SportPesa, ni mwezi mmoja na nusu umepita na imekuwa kama zawadi kubwa sana katika mikakati na mipango aliyonayo ya kimaendeleo.

Alisema kupitia bajaji hiyo, ataanza maisha mengine mapya kwani itamsaidia kuinuka kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wazazi wake, kupata ada ya kumlipia mtoto wake ambaye anasoma kidato cha sita, huku fedha nyingine atakazoingiza kupitia bajaji hiyo zikimsaidia kuanza kujenga nyumba ya kuishi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Abbas Tarimba, alisema: “Unaweza kuona kama miujiza vile, lakini mambo haya ni ya kweli kabisa na kila mtu anaweza kushinda na kumiliki bajaji kwa sababu SportPesa wanatoa bajaji moja kila siku kwa Mtanzania anayetupia ubashiri wake.

“Zoezi hili litachukua siku 100, yawezekana huu ndio wakati wako kuuaga umasikini na kuandika historia mpya. Piga *150*87# uanze kucheza na SportPesa au cheza kupitia tovuti www.sportpesa.co.tz. Hauhitaji simu ya kuchagua kwa sababu simu yoyote unaweza kucheza na SportPesa, iwe ya kitochi au smartphone. Cheza mara nyingi zaidi uongeze nafasi ya kushinda.”

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -