Saturday, November 28, 2020

MKENGE; Allardyce akubali aliingia mtegoni

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

kocha Sam Allardyce, amedai kwamba ‘waliomwekea mtego wamefanikiwa’ baada ya kukutana na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza tangu ameacha kibarua chake cha kuinoa timu ya Taifa ya England.

Allardyce aliacha kibarua hicho cha kuinoa England juzi Jumanne, baada ya kukiri mbele ya Chama cha Soka cha England (FA) kwamba madai yaliyotolewa na waandishi wa gazeti la Daily Telegraph yamefanya aonekane hastahili kuendelea kukinoa kikosi hicho.

Allardyce alizungumza na vyombo vya habari nyumbani kwake Bolton: “Ni wazi kwamba napaswa kufanya hivi kabla sijaenda popote. Ukitafakari hili ni jambo baya kufanya.

“Nilitaka kumsaidia mtu nilijua miaka 30 iliyopita kwamba ni kosa na kwa bahati mbaya nikakosea.

“Walionitega wameshinda kwa hili.”

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61 alichaguliwa kuwa kocha wa England siku 67 zilizopita na kuacha kazi hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili akiwa na rekodi ya kikosi chake kucheza mechi moja ambayo ilikuwa Septemba mwaka huu kwenye mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 dhidi ya Slovakia, ambayo waliibuka na ushindi.

Allardyce amedaiwa kujadili jinsi ya kukwepa sheria kuhusu uhamisho wa wachezaji, huku kipande cha video kikimwonyesha kocha huyo akimzodoa Roy Hodgson, akimwita Prince Harry ‘kijana mtukutu’ na akiwashutumu FA kwa ‘kupiga fedha’.

Pia gazeti hilo la Telegraph liliweka wazi kwamba alifanya makubaliano ya kusafiri Mashariki ya Mbali akilipwa kama balozi wa biashara hiyo ya uongo.

Akizungumza na Sky Sports jana, Allardyce alikanusha madai kwamba fedha ndicho kilichokuwa sababu ya wao kukutana, akisisitiza alifanya hivyo kama kuwasaidia marafiki zake hao.

“Makubaliano ya kuacha kazi yalifanyika kiurafiki na FA, naomba msamaha kwa FA na wote waliohusika kwa tukio hili ambalo nimejiingiza mwenyewe mkenge,” alisema Allardyce.

“Nina makubaliano ya siri, siwezi kujibu maswali mengine zaidi kwa sasa. Naenda mapumziko kutafakari.

“Nawatakia mafanikio mema Gareth Southgate (kocha wa muda wa England) na wachezaji wote wa England.”

Allardyce amethibitisha kwa Sky Sports kwamba hana mpango wa kuachana na soka na anatarajiwa kurejea kwenye kazi hiyo ya ukocha muda si mrefu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -