Friday, October 30, 2020

Mkhitaryan anapomuweka kitanzini Mourinho leo

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MANCHESTER, England

JOSE Mourinho si mfanyakazi pekee wa Manchester United anayeshtua wakazi wanaoishi pembeni ya hoteli ya Hotel. Yuko Henrikh Mkhitaryan!

Kila panapopambazuka, Henrikh Mkhitaryan huacha kitanda chake na kufungasha vifaa vyake kuelekea mazoezini.

Ndiye mchezaji anayewahi zaidi kufika katika viwanja vya Carrington kuliko yeyote yule, hata kifungua kinywa chake hupata akiwa mazoezini, si hotelini kama wengine.

Nyota huyu anayezungumza lugha sita ni rafiki wa kila mtu, wafanyakazi wa Carrington humpenda kwa utulivu na uchangamfu wake.

Lakini pamoja na yote haya, fundi huyu hana namba kwenye kikosi cha Manchester United. Licha ya Mourinho kutumia pauni mil 26.3 kumng’oa Borussia Dortmund, bado hajafahamu ni wapi atamtumia kwenye timu yake.

Mkhitaryan ameanza mchezo mmoja tu chini ya Mourinho – ule wa Manchester derby, wiki saba zilizopita ambapo aliishia kutolewa kipindi cha pili baada ya kuonyesha kiwango kibovu kwenye dakika 45 za kwanza.

Majeraha aliyopata akiwa na timu yake ya taifa ya Armenia yalimfanya kuzidi kukaa nje kwa muda mrefu bila kucheza.

Hata hivyo, Mourinho alieleza sababu iliyofanya amuweke benchi Mkhitaryan kwenye mchezo wa Kombe la Uropa dhidi ya Fenerbahce na ule wa ligi kuu dhidi ya Chelsea.

Mourinho alisema Mkhitaryan si majeruhi lakini bado hajawa fiti kuingia uwanjani, anatakiwa kufanya mazoezi kwa bidii kurudi katika ubora wake uliozoeleka.

Lakini mashabiki wa Man United hawakuridhishwa na majibu haya, wengi wanaamini anachofanyiwa Mkhitaryan ni sawa na kile Mourinho anachomfanyia kiungo mkongwe wa Ujerumani, Bastian Schweinsteiger.

Tofauti pekee ya wawili hawa, Mourinho alimsajili Mkhitaryan na Bastian alimkuta klabuni akiwa amesajiliwa na Louis van Gaal.

Nani asiyejua ubora wa Mkhitaryan? Ni miongoni mwa viungo bora kabisa barani Ulaya, msimu uliopita alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Bundesliga nchini Ujerumani baada ya kufunga mabao 23, asisti 20 kwenye michezo 51 aliyocheza.

Awali Henrick alikaribia kujiunga na Arsenal kabla ya United kuingilia kati na kuongeza kitita kuinasa saini yake.

Nyakati hizi Mkhitaryan huenda akawa kwenye majuto ya kwanini hakujiunga na Arsenal, chini ya Wenger huenda angepata muda mwingi wa kucheza.

Mashabiki wa United wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kumshawishi Mourinho kumrejesha Mkhitaryan kwenye kikosi cha kwanza wakiunda kampeni ya #freeMkhitaryan kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Na tayari uongozi wa United umekanusha vikali taarifa zinazozagaa kuwa watafanya biashara ya kumuuza fundi huyu wa mpira katika dirisha dogo la usajili, Januari mwakani.

Pia walikanusha uvumi kuwa walimsajili Mkhitaryan kwa shinikizo kutoka kwa wakala wake Mino Raiola ili waweze kuwapata nyota wengine wawili wanaomilikiwa na wakala huyo, Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic.

Uongozi pia unatambua kuwa Mkhitaryan ni aina ya wachezaji wanaotakiwa kuwa fiti kimwili na kiakili ili waweze kung’ara na hii ni baada ya nyota huyu kuwa na mwanzo mbaya pia wakati alipojiunga na Dortmund mwaka 2013.

Wanachotaka ni kuhakikisha Mkhitaryan anakuwa fiti na utayari wa asimilia 100 ndio wampe nafasi, kuliko kumharakisha akaharibu na kumpotezea kujiamini.

Daktari wa Man United, Steve McNally aliwaomba viongozi wa Armenia kutomuita kwenye kikosi chao Mkhitaryan ili aweze kupata muda mrefu wa kuzidi kuimarika.

Ni wiki ya nne sasa, Mkhitaryan anawahi mazoezini, anajituma kwa nguvu zake zote na bado hajaingia kwenye kikosi cha kwanza.

Zile dakika 45 dhidi ya Man City zimeendelea kuwa shubiri kwake mpaka leo. Wengi walitaraji angecheza dhidi ya Fenerbahce lakini Mourinho aliamua kuendelea kumpa muda wa kumpiza.

Ni wazi kila shabiki wa United amechoka kuvumilia kuona Mkhitaryan anaendelea kusugua benchi, wanamtaka uwanjani na bila shaka mchezo wa leo dhidi ya Burnley pale Old Trafford ndio sahihi zaidi kwake.

Kama Mourinho ataendelea kumuweka benchi tena na leo, bila shaka kelele zitakuwa kubwa mara mbili na hizi zinazovuma hivi sasa.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -