Tuesday, October 20, 2020

Mkhitaryan Kinachomtesa Old Trafford ni historia yake mwenyewe

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

MANCHESTER, England

MIONGONI mwa mastaa ambao usajili wao uliteka vichwa vya habari wakati wa majira ya kiangazi ni Henrikh Mkhitaryan.

Akitokea Borussia Dormund ya Bunderliga, kiungo huyo wa pembeni alitua Old Trafforrd kwa ada inayotajwa kuwa ni zaidi ya pauni milioni 20.

Kilichowashitua wengi si kiasi hicho kikubwa cha fedha, bali kipaji cha hali ya juu alichonacho staa huyo.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa soka, Mkhitaryan angekuwa na faida kubwa kwenye kikosi cha Man United ambacho kilionekana kuwa ‘nyanya’ msimu uliopita.

Kinyume na matarajio hayo ya wachambuzi, staa huyo ameshindwa kupenya na kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Man United.

Kutokana na hilo, mashabiki wengi wa soka, hasa wale wa Man United watakuwa wakiumiza kichwa kujiuliza kile kilichomsibu staa wao huyo.

Tangu alipotua jijini Manchester, Mkhitaryan amefeli kuthibitisha ubora wake ulioifanya Manchester United kumsajili.

Katika michezo 13 ya mashindano yote msimu huu, Mkhitaryan ameingia mara moja kwenye kikosi cha kwanza.

Mchezo huo alioingia kwenye kikosi cha kwanza ni ule wa ‘Manchester derby’ dhidi ya mahasimu wao, Manchester City.

Mkali huyo mwenye umri wa miaka 27 hakuwa kwenye ubora aliotoka nao Dortmund, kwani alipoteza mipira mara 12.

Kwa kufanya hivyo, Mkhitaryan alikuwa mchezaji aliyeshindwa kumiliki mpira kuliko wote waliokuwa uwanjani.

Ilishangaza kuona Mourinho akimwacha uwanjani hadi pale kipindi cha kwanza kilipomalizika.

Historia inaonesha kuwa imekuwa ni kawaida kwa Mkhitaryan kushindwa kufanya vizuri msimu wake wa kwanza katika klabu zote alizopitia.

Alikumbana na upepo huo alipokuwa na Shakhtar Donetsk ya Ukraine na mambo yalikuwa hivyo pia alipojiunga na Borussia Dortmund.

Kwa mujibu wa aliyekuwa kocha wake katika klabu ya Shakhtar, Mircea Lucescum, Mkhtaryan alipitia kipindi kigumu akiwa klabuni hapo kabla ya kuibuka na kuwa moto wa kuotea mbali misimu kadhaa baadaye.

“Haikuwa rahisi kwake hapo mwanzoni, aliteseka kuweza kuwa kwenye kiwango cha juu,” alisema Lucescu.

Mkhitaryan alianza kutema cheche katika msimu wake wa pili klabuni hapo ambapo ambapo alipachika mabao 25.

Lakini pia, Mkhitaryan aliposajiliwa na Borussia mwaka 2013, aliyekuwa kocha wa kikosi hicho ambaye hivi sasa anainoa Liverpool, Jurgen Klopp, alimtega.

Klopp aliweka mezani euro 50 na kumtaka staa huyo kufunga mabao saba pekee ili aweze kuchukua kiasi hicho cha fedha.

Kama angeshindwa kufanya hivyo pamoja na kupiga mashuti 30, Klopp angerudisha mfukoni mpunga huo.

Kauli ya kocha wake huyo ilitokana na kiwango kibovu alichokuwa nacho Mkhtaryan kwa kipindi hicho.

Hata hivyo, mbali na Mkhtaryan, kikosi chote cha Dortmund hakikuwa sawa.

Kilikuwa na mwendo wa kusuasua kwenye mbio za kuwania taji la Bundersliga na kiliondoshwa na Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Tatizo kubwa ni kwamba nilitoka kwenye ligi ambayo huwezi kuilinganisha na Bundesliga,” alisema kiungo huyo.

“Pale Shakhtar, mechi zinafana. Timu pinzani zinazuia sana, mara kwa mara tulikuwa tukimiliki mipira na kama tungekuwa wa kwanza kupata bao, mchezo ungeishia hapo.

“Hapa Ujerumani haikuwa hivyo. Hata timu zinazoburuza mkia zinaweza kukupa tabu.”

Mkhitaryan alikuwa akicheza kama winga wa kulia kwa kipindi chote alichokuwa Dortmund.

Kwa kucheza nafasi hiyo, msimu uliopita, nyota huyo aling’ara na kuwa kinara wa ‘asisti’ Bundesliga.

Lakini pia, alicheka na nyavu mara 23 katika mechi za mashindano mbalimbali.

Mafanikio hayo yalimwezesha kunyakua tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Jarida la Kicker.

Kwa upande wake, Kocha wa Man United, Jose Mourinho, anaamini kuwa hajapotea kumnunua nyota huyo, licha ya kuanza kwa mwendo wa kusuasua.

Mourinho amedai kuwa kinachohitajika kwa sasa ni kumpa muda Mkhitaryan kabla ya kuanza kushuhudia ‘mavituz’ yake.

“Kwa sababu najua kabisa (Mkhitaryan) ni mchezaji mzuri na sina shaka kuwa atafanikiwa,” alisema Mourinho.

“Sina haraka ya kumuona akiingia uwanjani kwa dakika zote za kila mechi, nataka kuonesha watu ni jinsi gani alivyo mchezaji bora,” alisema Mourinho.

Mbali na Mourinho, Klopp wa Liver naye ameonyesha imani yake kwa Mkhitaryan, akisema ni muda tu unaosubiriwa kabla ya nyota huyo wa kimataifa wa Armenia kuanza kazi zake Ligi Kuu England.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -